Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini: Marekani itajuta

Serikali ya Korea Kaskazini imekashifu vikali vikwazo vipya ilivyowekewa na baraza la usalama la umoja wa Mataifa kutokana na majaribio yake ya silaha za nyuklia iliyoyafanya hivi karibuni, nchi hiyo ikitishia kulipa kisasi dhidi ya utawala wa Washington ambao inaulaumu kwa kushinikiza vikwazo hivyo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini ainyo Marekani kutoendelea kuitishia kuishambulia kijeshi.
Kiongozi wa Korea Kaskazini ainyo Marekani kutoendelea kuitishia kuishambulia kijeshi. KCNA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Korea Kaskazini kwenye umoja wa Mataifa Han Tae Song, ameikashifu nchi ya Marekani aliyosema ilitengeneza taarifa za uongo ili kuiumiza nchi yake na kwamba hatua hiyo haitaachwa ipite bila kulipa kisasi.

Bw. Tae Song ameishutumu Marekani kwa kutafuta makabiliano ya kisiasa , kiuchumi na kijeshi.

Han Tae Song alisema amekataa kile alichokitaja kuwa vikwazo vilivyo kinyume na sheria.

Akizungumza baada ya kudhinishwa kwa vikwazo hivyo, balozi wa Marekani Nikki Haley amesema baraza hilo limeonesha mshikamano katika kuizuia Korea kaskazini kuwa tishio kwa usalama wa dunia.

Mapema Marekani iliapa kuweka shinikizo zaidi ikiwa Korea Kaskazini itaendela na njia zake hatari.

Miongoni mwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo ni pamoja kuzuiwa kuagiza mafuta ghafi kutoka nje, gesi na uuzaji wa nguo hali ambayo wadadisi wa mambo wanasema itaathiri pakubwa uchumi wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.