Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini yashindwa kurusha kombora

Korea Kaskazini imeshindwa katika jaribio lake kufyatua kombora Ijumaa asubuhi kuadhimisha miaka ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung, jeshi la korea Kaskazini na afisa mwandamizi katika wizara ya Ulinzi ya Marekani wametangaza.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, Pyongyang Februari 13, 2016.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, Pyongyang Februari 13, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Il-sung.

Siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Korea Kaskazini, babu yake Kim, huwa muhimu sana kwa taifa hilo. Miaka minne iliyopita, Korea Kaskazini ilijaribu kusherehekea kwa kuzindua kombora lakini juhudi hizo zikafeli.

"Korea Kaskazini inaonekana kuwa imejaribu kufyatua kombora karibu na pwani yake ya mashariki mapema Ijumaa asubuhi lakini inaonekana kuwa imeshindwa," wamesema wakuu wa majeshi ya Korea Kusini katika taarifa yao.

"Korea ya Kaskazini imejaribu kurusha kombora saa 2:33 saa za kimataifa" Alhamisi, lakini jaribio hilo "limefeli," afisa mwandamizi katika Wizara ya ulinzi ya Marekani, ambaye hakutaka jinalake litajwe, amesema.

Bado haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa jaribio hilo lilikuwa la kombora la masafa ya wastani kwa jina la “Musudan” ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia jaribio.

Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, likinukuu duru za serikali, limesema kombora hilo lilikuwa aina ya kombora la Musudan, ambalo kitaalamu hujulikana kama BM-25.

Kombora hilo linaweza kufika umbali wa kilomita 3,000 na kufikia kambi ya majeshi ya Marekani iliyopo kisiwa cha Guam katika bahari ya Pasifiki. Lakini haliwezi kufika nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.