Pata taarifa kuu
KOREA YA KASKAZINI-KOREA YA KUSINI-MAREKANI

Korea ya Kaskazini yatishia Korea Kusini na Marekani

Pyongyang imetishia kufanya mashambulizi ya kinyuklia dhidi ya Korea Kusini na Marekani, ikiwa nchi hizi zitaamua kufanya mazoezi yao ya pamoja ya kijeshi yaliopangwa kuanza Jumatatu hii.

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong-un wakati wa mazoezi ya kijeshi, mwezi Disemba 2014.
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong-un wakati wa mazoezi ya kijeshi, mwezi Disemba 2014. REUTERS/KCNA/Files
Matangazo ya kibiashara

Mazoezi haya ya kijeshi ni muhimu zaidi katika historia ya muungano wao. Maonyesho ya kijeshi yataendeshwa skwa kuheshimu serikali ya Korea Kaskazini, ambayo mapema mwanzoni mwa mwaka huu ilifanya jaribio la nyuklia na jaribio la kurusha angani kombora la kinyuklia.

Tishio la "shambulizi la nyuklia la kujilinda kulingana na sheria", maneno haya yamo katika tangazolililotolewa na uongozi mkuu wa jeshi la Korea ya Kaskazini, shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA, limearifu JUmatatu hii.

Matamshi haya yanakuja siku chache tu baada ya uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka mfululizo mpya wa vikwazo vigumu dhidi ya Korea Kaskazini baada majaribio ya hivi karibu ya nyuklia na urushwaji anagani wa komboraviliotekelezwa na utawala wa kikomunisti.

Katika taarifa yake ilionukuliwa na KCNA, uongozi mkuu wa jeshi la Korea ya Kaskazini umesema kuwa vikwazo "viovu" imepelekea "nchi hii kumomonyoka kama udongo unaokabiliwa na mapigano."

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi

Ukishtumu mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka ya Washington na Seoul kuwa ni "mazoezi ya kivita ya nyuklia ambayo yamejificha," uongozi mkuu wa kijeshi umeonya: "Kama tukibonyeza kwenye vifaa kwa kuwaangamiza maadui zetu (...), vyanzo vyote vya uchokozi vitapungua papo hapo kwa bahari za moto na majivu. "

Mazoezi haya yanahusu hasa maandalizi yanayowezekena ya operesheni za kujilinda zenye malengo ya kuzuia Korea ya Kaskazini kutumia silaha za maangamizi. Haya ni mazoezi muhimu zaidi kuwahi kufanywa na washirika wawili, mwandishi wetu mjini Seoul, Frédéric Ojardias, amesema. Askari 300,000 wa Korea Kusini na 15,000 wa Marekani watashiriki katika mazoezi mbalimbali ya kijeshi katika katika nchi kavu, baharini na angani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.