Pata taarifa kuu
UNSC-KOREA KASKAZINI-VIKWAZO

UNSC yapitisha vikwazo vigumu dhidi ya Korea ya Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano hii, limeiwekea duru mfululizo mpya wa vikwazo vigumu dhidi ya Korea Kaskazini baada ya majaribio ya hivi karibuni ya nyuklia na makombora yalioendeshwa na utawala wa kikomunisti.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mjini Geneva, Uswisi, Februari 29, 2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mjini Geneva, Uswisi, Februari 29, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Azimio la Baraza, lililoyowasilishwa na Umoja wa Mataifa, limepitishwa kwa kauli moja, ikiwa ni pamoja China, ambayo ni mshirika wa Pyongyang.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, hivi karibuni, alikaidi kwa mara nyingine jumuiya ya kimataifa akiwataka wanasayansi wake kurusha satelaiti zaidi, wiki moja baada ya kurusha chombo angani, kitendo kilichotuhumiwa na mataifa ya kigeni.

Katika karamu ilioandaliwa kwa kuwapongeza watafiti, wataalamu na maafisa wa mpango wa mambo ya anga wa Korea Kaskazini Februari 7, Kim alibainisha kuwa harakati hiyo ilitokea "katika kipindi kigumu ambapo vikosi vya waasi vimeendelea na harakati zao" ili kuididimiza "Korea Kaskazini", shirika la habari la serikali la KCNA limearifu leo Jumatatu.

Mwezi mmoja baada ya kufanya jaribio lake la nne la kinyuklia, lililoshtumiwa na jumuiya ya kimataifa, Korea Kaskazini imezitia wasiwasi nchi za kigeni kwa kurusha kwa mara nyingine tena chombo chake cha Kwangmyongsong-4.

Urushaji huo ulichukuliwa kama jaribio la kombora, katika ukiukaji wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini alisema uzinduzi huo ulifanikiwa kwa sababu ya "kujiamini kabisa" kwa timu iliyoteuliwa kutoka chama tawala, na kuongeza kuwa jasho la wanasayansi lilikua kama mafuta muhimu ya chombo hicho.

Wakati huo alwapongeza wafanyakazi wa mpango wa mambo ya anga wa Korea Kaskazini kwa kutumia mafanikio haya kama ufanisi zaidi "kuelekea malengo ya juu na hivyo kuzindua satelaiti zaidi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.