Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-JARIBIO

Kiongozi wa Korea Kaskazini ataka satelaiti zaidi zirushwe angani

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, amekaidi kwa mara nyingine jumuiya ya kimataifa akiwataka wanasayansi wake kurusha satelaiti zaidi, wiki moja baada ya kurusha chombo angani, kitendo kilichotuhumiwa mataifa ya kigeni.

Picha Zilizotolewa Februari 7, 2016 na shirika la habari la serikali la Korea ya Kaskazini (KCNA) zikionyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un akihudhuria katika eneo lisilojulikana, zoezi la kurusha roketi ya kubebachombo angani.
Picha Zilizotolewa Februari 7, 2016 na shirika la habari la serikali la Korea ya Kaskazini (KCNA) zikionyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un akihudhuria katika eneo lisilojulikana, zoezi la kurusha roketi ya kubebachombo angani. AFP/KCNA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika karamu ilioandaliwa kwa kuwapongeza watafiti, wataalamu na maafisa wa mpango mambo ya anga wa Korea Kaskazini Februari 7, Kim alibainisha kuwa harakati hiyo ilitokea "katika kipindi kigumu ambapo vikosi vya waasi vimeendelea na harakati zao" ili kuididimiza "Korea Kaskazini", shirika la habari la serikali la KCNA limearifu leo Jumatatu.

Mwezi mmoja baada ya kufanya jaribio lake la nne la kinyuklia, lililoshtumiwa na jumuiya ya kimataifa, Korea Kaskazini imezita wasiwasi nchi za kigeni kwa kurusha kwa mara nyingine tena chombo chake cha Kwangmyongsong-4.

Urushaji huo unachukuliwa kama jaribio la kombora, katika ukiukaji wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema uzinduzi huo ulifanikiwa kwa sababu ya "kujiamini kabisa" kwa timu iliyoteuliwa kutoka chama tawala, na kuongeza kuwa jasho la wanasayansi lilikua kama mafuta muhimu ya chombo hicho.

Amewapongeza wafanyakazi wa mpango wa mambo ya anga wa Korea Kaskazini kwa kutumia mafanikio haya kama ufanisi zaidi "kuelekea malengo ya juu na hivyo kuzindua satelaiti zaidi."

Washington, Seoul na Tokyo wako katika mstari wa mbele kwa itihada za kidiplomasia za kulishinikiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzidisha vikwazo zaidi dhidi ya Pyongyang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.