Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Picha za Satellite zaonesha Korea Kaskazini kukamilisha mtambo wake wa kurusha roketi

Satellite za Marekani zimeonesha kuwa nchi ya Korea Kaskazini huenda ikawa imeanza kuandaa roketi yake inayotarajiwa kuirusha hivi karibuni, wakati huu ambapo jumuiya ya kimataifa imeeleza kuguswa na tangazo la utawala wa Pyongyang.Β 

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un REUTERS/KCNA/Files
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Pyongyang ulitangaza kuwa utafanya jaribio jingine la kombora la masafa marefu kati ya February 8 hadi 25 mwaka huu, ikiwa ni kipindi ambacho pia ni maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya kuzawaliwa kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-Il.

Nchi ya Korea Kaskazini inasisitiza majaribio ya roketi zake ni majaribia ya kisayansi, lakini Marekani na washirika wake wakiwemo Korea Kusini wanaseam kuwa roketi hiyo ni muendelezo wa nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia.

Taarifa ya wizara ya mambo ya ndani inasema kuwa, picha za Satellite zimeonesha kuwa huenda matayarisho ya kufanyika kwa jaribio hilo, yakakamilika ndani ya siku chache zijazo.

Marekani inasema toka Alhamisi ya wiki hii, picha zinaonesha kuongezeka kwa idadi ya watu kwenye eneo ambako jaribio hilo litafanyika, huku pia magari na vifaa vikionekana kuingia.

Korea Kaskazini imeshatangaza kuwa haitaruhusu roketi ya aina yoyote kutoka Korea Kaskazini kupita kwenye anga yake na kwamba haitasita kuidungua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.