Pata taarifa kuu

Korea Kusini yakemea jaribio la kurushwa kwa makombora mawili na Korea Kaskazini na kudaikuwa ni uchochezi

Korea ya Kaskazini imerusha makombora baharini katika pwani yake ya mashariki kwa mara ya pili hii leo , hatua iliyosababisha korea kusini kutoa onyo kwa taifa hilo kuacha uchochezi.Majaribio hayo ya makombora ni wazi yamegongana na mazoezi ya mwaka yanayofanywa na Marekani na korea kusini ambayo yamesitishwa juma lililopita na kupelekwa mbele hadi katikati ya mwezi April.

Majaribio la Makombora ya masafa mafupi
Majaribio la Makombora ya masafa mafupi
Matangazo ya kibiashara

Makombora mawili yalirushwa mapema hii leo na kusafiri kilometa mia tano katika bahari ya japani kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya korea kusini.

Makombora ya masafa mafupi yalirushwa kwa mtindo huo alhamisi juma lililopita.

Makombora hayo yaliorushwa leo Jumatatu, yanafanana na Scuds yaliorushwa juma lililopita. Makombora aina ya Scuds ni makombora yenye vyombo vifupi lakini yanaweza kurushwa hadi kwenye masafa marefu.

Makombora hayo aina ya Scuds yanaweza kufika katika kituo chcochote nchini Korea Kusini. Korea Kusini awali ilitumia makombora kama hayo ili kubainisha hasira yao dhidi ya hatuwa hiyo ya majaribio ya kijeshi

Majaribio ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kaskazini yalianza tangu Februari 25 licha ya korea Kusini kupinga hatuwa hiyo ikisema kwamba ni njama cha uchochezi na mpango wa kuvamia kisiwa cha Penensula.

Katika hatuwa ya kwanza, Jeshi la Marekani Pentagone, ilifahamisha kwamba Korea Kaskazini inaruhusiwa kufanya majaribio ya makombora aina ya Scud yenye masafa mafupi. Lakini siku ya Ijumaa juma lililopita Marekani ikarejelea kauli yake hiyo na kuthibitisha kwamba urushwaji wa makombora hayo unavunja azimia la Umoja wa Mataifa inayopinga matumizi ya makombora ya aina hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.