Pata taarifa kuu
URUSI-IRAN-UNSC-VIKWAZO

Moscow yapinga vikwazo dhidi ya Tehran

Urusi imetangaza Jumatatu hii kuwa inapinga vikali vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran kwa ajili ya majaribio yake ya hivi karibuni ya kombora, ikibaini kwamba majaribio hayo hayakiuki maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Vladimir Putin, wakati wa mkutano wake wa jadi wa kila mwaka na waandishi wa habari mjini Moscow tarehe 17 Desemba mwaka 2015.
Vladimir Putin, wakati wa mkutano wake wa jadi wa kila mwaka na waandishi wa habari mjini Moscow tarehe 17 Desemba mwaka 2015. REUTERS/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

"Kwa neno moja, jibu liko wazi ni, hapana," Balozi wa Urusi katika Baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin, amewajibu waandishi wa habari ambao wamekua wakimhoji kuhusu vikwazo hivyo, kabla ya mashauriano katika Umoja wa Mataifa juu ya suala hili lililodaiwa na Marekani.

Urusi, mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ina kura ya turufu juu ya uamuzi wowote. Wanadiplomasia wanasema China, pia mjumbe wa kudumu, au Venezuela, pia wanasita kuiwekea Iran vikwazo.

Marekani iliomba baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa kuandaa kikao cha mashauriano ili kujadili "urushaji hatari" wa makombora ya masafa marefu uliotekelezwa na Iran, majaribio ambayo, kwa mujibu wa Marekani na washirka wake yanakiuka azimio 2231.

Chini ya azimio hilo, Iran bado inajiepusha na uzinduzi wamakombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kuwa na vifaa hatari vya nyuklia, hata kama vikwazo vya kimataifa dhidi ya Tehran viliondolewa chini ya mkataba wa nyuklia ulioafikiwa Julai mwaka jana na mataifa yenye nguvu na kuanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Iran imekanusha kuwa ina nia ya kupata silaha za nyuklia na imesema kuwa makombora yake hayajatengenezwa ili kisafirisha bomu la atomiki.

utawala wa Kishia ulibaini kwamba wiki iliyopita ulitekeleza mfululizo wa majaribio ya kurusha angani makombora ya masafa marefu. afisa mmoja wa kijeshi wa Iran amesema makombora hayo yanawezakurushwa hadi Israel.

Muda mfupi kabla ya mkutano wa Baraza la Usalam ala Umoja wa Mataifa, balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Danny Danon, ametoa wito kwa nchi 15 wanachama "kutekeleza hatua za kuadhibu zilio wazi" dhidi ya Tehran kuipa "ujumbe wa wazi".

"Kama Baraza la Usalama halitoochukua hatua madhubuti (...) tutakuwa tumeiruhusu Iran kuendelea majaribio yake ya makombora," Danny Danon ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.