Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAN-USHIRIKIANO

Paris na Tehran zaanzisha "Uhusiano mpya" na kusaini mikataba

Iran na Ufaransa zimetangaza Alhamisi hii "uhusiano mpya" wakati wa ziara rasmi ya Rais wa Iran Hassan Rouhani mjini Paris, ziara ambayo imeongozwa na mikataba ya kiuchumi ya mabilioni ya Euro na kubadilishana ushirikiano wa kidiplomasia kuhusu Syria.

Rais François Hollande (kulia) akimkaribisha Rais wa Iran Hassan Rouhani, Januari 28, 2016 katika Paris.
Rais François Hollande (kulia) akimkaribisha Rais wa Iran Hassan Rouhani, Januari 28, 2016 katika Paris. BERTRAND GUAY/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Huu ni ukurasa mpya katika uhusiano wetu, ambao unaanzishwa leo," Rais wa Ufaransa François Hollande, akiambatana na mwenzake wa Iran, amehakikisha katika mkutano na waandishi wa habari mjini Paris.

"Tusahau tofauti zetu", alisema mapema asubuhi Rais wa Iran Hassan Rouhani, akitoa wito kwa "Uhusiano mpya" na kufurahia "hali chanya" iliyoletwa na kuondoelwa kwa vikwazo dhidi ya nchi yake kwa kuleta "nguvu mpya" kwa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Tangu mwaka mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979, mahusiano kati ya Tehran na Paris yalikumbwa na migogoro mingi hadi mwezi Julai kulikopatikana makata wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Wakati huo huo Mkataba wa kiitifaki kwa Iran kununua ndege 118 aina ya Airbus kutoka kampuni ya Ulayaumehitimishwa kwa kiasi cha Dola bilioni 25.

Kampuni kubwa ya mafuta TOTAL imesaini mkataba wa kununua mjini Tehran "kati ya mapipa 150,000 na 200,000 kwa siku" ya mafuta yasiyosafishwa. Iran ina hifadhi nne duniani ya dhahabu nyeusi na inauza katika nchi za kigeni zaidi ya mapipa milioni moja kwa jumla ya milioni 2.8 inayotengenezwa kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.