Pata taarifa kuu

Zaidi ya Wafaransa 170 na wageni 70 waondolewa na Ufaransa kutoka Haiti

Zaidi ya Wafaransa 170 na baadhi ya Wazungu 70 na raia wengine wa kigeni wamehamishwa kutoka Haiti, nchi iliyotumbukia katika machafuko, ndani ya helikopta za jeshi la Ufaransa, Wizara ya Mambo ya Nje imetangaza Jumatano Machi 27.

Mabaki ya magari yaliyoungua karibu na karakana huko Port-au-Prince, Haiti, Machi 25, 2024.
Mabaki ya magari yaliyoungua karibu na karakana huko Port-au-Prince, Haiti, Machi 25, 2024. AFP - CLARENS SIFFROY
Matangazo ya kibiashara

Hawa ni watu walio "katika mazingira magumu" ambao walihamishwa kutoka Haiti "kwenye meli ya Jeshi la taifa la Wanamaji ambalo litawasafirisha leo hadi Fort-de-France", inabainisha Quai d'Orsay katika taarifa. Tangu Jumapili Machi 24, vikosi vya jeshi vya Ufaransa vimewajibika kwa shughuli za kuwahamisha raia. Zoezi hili linafanywa na helikopta kutoka ardhini hadi kwenye meli ya jeshi la taifa la wanamaji. Watu wanaohamishwa husafirishwa hadi Fort-de-France huko Martinique.

"Tuliteswa na uporaji, magari kuchomwa, kuharibiwa, kuibiwa ..."

Siku ya Jumatatu, zaidi ya raia wa Ufaransa waliojiandikisha kuondoka kwa hiari yao walilazimika kungoja zaidi ya ilivyotarajiwa, kwa sababu za usalama, katika shule ya upili ya Ufaransa. Christophe, raia wa Ufaransa aliyehojiwa akiwa huko Port-Au-Prince na Michel Gendre kutoka Outre-mer La 1ʳᵉ, anashuhudia: "Nilifika Haiti mnamo Desemba 4, tulilazimika kufunga kampuni tangu Februari 29 na, wiki iliyopita, tuliibiwa, magari yalichomwa moto, kuharibiwa, kuibiwa ... Kwa hiyo, nilikuwa katika majadiliano na uongozi wangu mkuu ambao walipendelea kuniambia niondoke, kwa sasa, mpaka utulivu urudi. Bado kuna askari wachache wa Ufaransa. Nilizungumza na baadhi yao, mmoja wao, kwa muda mrefu sana, aliniambia: "Usijali. Tuna bastola tu, lakini ikiwa itabidi tupigane, tuna silaha nzito." Kwa nadharia, tunaelekea Fort-de-France, ndivyo nilivyoambiwa. Na kisha tutakwenda Paris kwa kutumia ndege ya kibiashara. Lakini lini? Sijui. "

Baadhi ya Wafaransa 1,100, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya raia walio na uraia pacha, wanaishi Haiti, kulingana na wizara. "Ubalozi wa Ufaransa huko Port-au-Prince unaendelea kufanya kazi na unaendelea kuhamasishwa kikamilifu kuunga mkono jamii ya Wafaransa wanaoishi nchini Haiti," inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari ya Machi 27.

Haiti, ambayo tayari ni mwathirika wa mzozo mkubwa wa kisiasa na kiusalama, imekumbwa na ghasia mpya tangu mwanzoni mwa mwezi huu, huku magenge kadhaa yakiwa yameungana kushambulia maeneo ya kimkakati huko Port-au-Prince. Waziri Mkuu Ariel Henry alikubali kujiuzulu mnamo Machi 11. Tangu wakati huo, mazungumzo yamekuwa yakiendelea kuunda mamlaka ya mpito. Wakati huo huo, magenge yenye silaha yanazidisha mashambulizi yao katika mji mkuu wa Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.