Pata taarifa kuu

Haiti: Nchi inazidi kuzama katika machafuko na vurugu

Haiti inazidi kuzama katika machafuko na vurugu za magenge. Wakati Baraza la rais likijitahidi kujiweka sawa, jana Jumatatu Machi 18, mashambulizi ya makundi yenye silaha yaliendelea, hasa katika mtaa wa Pétion-Ville, katika viunga vya kusini mwa Port-au-Prince. Kinachoongezwa kwa hili ni mashambulizi kwenye mitambo ya umeme, na kusababisha kukatika kwa umeme katika mji mkuu.

Katika moha ya mitaa ya Port-au-Prince, Machi 12, 2024.
Katika moha ya mitaa ya Port-au-Prince, Machi 12, 2024. AFP - CLARENS SIFFROY
Matangazo ya kibiashara

Port-au-Prince "imetumbukia kwenye giza", ni kichwa cha habari kwenye tovuti ya habari ya Alterpresse asubuhi ya leo. Mitambo kadhaa ya umeme pamoja na kituo cha umeme cha Varreux viliharibiwa au kuharibiwa vibaya. Makundi yenye silaha pia yaliendelea na mashambulizi yao dhidi ya taasisi za serikali.

Benki Kuu yalengwa

Jana, Jumatatu Machi 18, Benki Kuu ya Haiti ililengwa na shambulio ambalo lilizuiwa na polisi. Na wakati wa shambulio la makazi kadhaa katika vitongoji tajiri vya wilaya ya Petion-Ville, angalau watu kumi na wanne waliuawa. Wakati magenge yanadumisha shinikizo kwa mji mkuu ambao wanadhibiti karibu 80% ya mji mzima, zoezi la kuanzishwa kwa Baraza la Rais limechelewa.

Baraza la Rais mwishoni mwa wiki

Yote haya ni kutokana na mifarakano ndani ya makundi ambayo yalitakiwa kutuma wawakilishi kwa chombo hiki kinachopaswa kuteua Waziri Mkuu wa mpito. Hadi sasa, Jumuiya ya Mataifa ya Karibiani (CARICOM), ambayo inasimamia mazungumzo ya Haiti, imepokea majina sita ya wawakilishi saba wanaotakiwa kusimamia baraza hili la rais. Chama cha kisiasa kilikataa kushiriki katika Baraza la rais ambalo, kulingana na taarifa kutoka Radio Télé Métronome, linaweza kuanzishwa mwishoni mwa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.