Pata taarifa kuu

Donald Trump na Joe Biden wahakikishiwa kushinda uteuzi wa vyama vyao

Baada ya siku nyingine ya uchaguzi wa mchujo, Jumanne Machi 12, haswa huko Georgia, Joe Biden na Donald Trump wamepata idadi ya kutosha ya wajumbe kushinda uteuzi wa vyama vyao: kwa hivyo wagombea hao wawili watakabiliana mnamo mwezi wa Novemba 2024 kwa uchaguzi wa urais wa Marekani.

Joe Biden na Donald Trump, washinda na kuingia katika uteuzi wa vyama vyao kuwania uchaguzi wa urais mwezi Novemba 2024.
Joe Biden na Donald Trump, washinda na kuingia katika uteuzi wa vyama vyao kuwania uchaguzi wa urais mwezi Novemba 2024. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Bango la pambano la urais halikuwa na shaka tena, wagombea hao wawili wameondoa ushindani katika kinyang'anyiro cha uteuzi. Sasa imethibitishwa kihisabati, anaripoti mwandishi wetu huko Miami, David Thomson. Baada ya siku hii mpya ya uchaguzi wa mchujo wa Republican na Democratic, Joe Biden na Donald Trump kila mmoja amepata kizingiti cha wajumbe wanaohitajika kuteuliwa na vyama vyao kama wagombea kwa uchaguzi wa urais wa Novemba wakati wa makongamano yatakayofanyika majira ya joto. Kampeni ya urais kati ya Joe Bien na Donald Trump sasa inaweza kuanza kwa dhati, hata kama Wamarekani wengi hawataki pambano hili la marudio.

Washington, Mississippi na Hawaii zilipiga kura siku ya Jumanne, na vile vile Georgia, jimbo la kimkakati, mojawapo ya majimbo haya muhimu yenye maamuzi ya kushinda uchaguzi wa urais wa Marekani. Jimbo ambalo Donald Trump alishinda mnamo 2016 lakini pia na Joe Biden mnamo 2020, na kupata chini ya kura 12,000 dhidi ya mshindani wake. Kura hizi 12,000 ambazo Donald Trump alikuwa amewaomba maafisa wa eneo hilo kumtafutia ili kutengua matokeo ambayo sasa ni maarufu nchini Marekani na ambayo yalisababisha ashtakiwe na mwendesha mashtaka wa Atlanta kwa kujaribu kunyang'anya uchaguzi mwaka wa 2020.

Karibu miezi minane ya kampeni

Rais aliye madarakani Joe Biden alivuka kizingiti cha wajumbe 1,968 waliohitajika kwa kushinda mchujo wa chama cha  Democratic katika jimbo la Georgia. Kuhusu Donald Trump, 77, ushindi wake katika Jimbo la Washington ulimwezesha kuvuka kizingiti cha wajumbe 1,215 muhimu kushinda uteuzi wa Chama cha Republican.

Wanaume hao wawili kwa hivyo wanajiandaa kurudia pamano la 2020. "Nina heshima kwamba muungano mpana wa wapiga kura wanaowakilisha aina mbalimbali tajiri za Chama cha Democratic kote nchini wameweka imani yao kwangu kwa mara nyingine tena kuongoza chama - na nchi - wakati ambapo tishio linaloletwa na Trump ni kubwa kuliko wakati mwingine wowote,” Hoe Biden amesema katika taarifa yake.

Ikiwa kuapishwa tena mapema kwa rais anayeondoka ni jambo la kawaida, ushindi wa rais huyo wa zamani wa chama cha Republican katika takriban chaguzi zote za mchujo za chama cha Republican hadi sasa umemwezesha kupata uteuzi huo mapema zaidi kuliko wagombea wengi wa upinzani wakati wa kampeni zilizopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.