Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Marekani yakumbwa na maandamano mengi kuunga mkono Gaza

Marekani inaendelea kukumbwa na maandamano a watru wenye hasira kufuatia vita vinavoendelea katika Ukanda wa Gaza. Maelfu ya Wamarekani wameandamana hivi punde katika miji mindi kote nchini, kutoka Washington hadi Los Angeles, Jumamosi Machi 2, kudai kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.

Mwanamume huyu akiwa ameshika bendera wakati wa maandamano yanayounga mkono Wapalestina, katika Jiji la New York, Marekani, Machi 2, 2024.
Mwanamume huyu akiwa ameshika bendera wakati wa maandamano yanayounga mkono Wapalestina, katika Jiji la New York, Marekani, Machi 2, 2024. © David Dee Delgado / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Waandamanaji kutoka doni zote na jamii mbalimbali wameandamana wakiwa na mabango yaliyoandikwa "lazima vita vikoe Gaza". Kutoridhika kwa umma wa Marekani kumefikia kiwango kipya kwani wiki iliyopita mwanajeshi alijichoma moto karibu na Ikulu ya White House kupinga "mauaji ya halaiki dhidi ya raia wa Palestina." Jumamosi hii alasiri, mamia ya watu waliobebelea miavuli yalimiminika katika eneo la Washington Square, mjini New York, ambapo wakazi wa Big Apple walikuja kwa wingi.

Mary, 63, hajakosa maandamano tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Anataka utawala wa Biden kuishinikiza serikali ya Netanyahu kusitisha uhasama, na uidhinishaji wa misaada halisi ya kibinadamu kwa Gaza. “Kama mfuasi mkuu wa kifedha wa serikali ya sasa ya Israel, sauti hii lazima itoke Marekani. Ninamuunga mkono Rais Biden. Mimi ni mwanachama wa Chama cha Democratic, na nadhani amefanya mambo mengi mazuri. Lakini katika kesi hii, lazima achukue msimamo thabiti zaidi, "anaelezea mama huyo mwenye umri wa miaka sitini. Hata kama amekatishwa tamaa na Joe Biden, Mary bado atampigia kura mwezi Novemba mwaka huu, ili asimpe Donald Trump nafasi hiyo. Lakini hii sivyo ilivyo kwa kila mtu.

Wapiga kura wenye hasira

Wapiga kura wengi, waliompigia kura mwaka wa 2020, wanataka kumchukulia hatua mwaka wa 2024. Wakati mwingine tayari walikuwa hawajaridhishwa na sera zake kuhusu uhamiaji, Usalama wa Jamii... lakini ni uungwaji mkono usio na masharti kwa Israel ambao uliwafanya kubadili mawazo yao. Elsa ana asili ya Asia, na kama watu wengi walio wachache hapa, anajitambulisha na Wapalestina wanaoshambuliwa. "Nadhani ina athari kwa jinsi watu wengi wanavyopiga kura. Siku zote wanadhani watapata kura zetu, labda si zetu, zile za vijana. Wanategemea kura za wazee, lakini tutajitokeza kwa wingi na kuwaonyesha kwamba tunajali, na kwamba sauti zetu zinahesabiwa,” anatumai.

Uungwaji mkono huu wa Marekani kwa Israel ndio hakika utakuwa na athari kubwa kwenye kampeni ya Joe Biden. Hata kama kwa sasa, rais wa Marekani na timu yake wanakataa kuamini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.