Pata taarifa kuu

Mwanajeshi wa Marekani afariki baada ya kujichoma moto nje ya ubalozi wa Israel mjini Washington

Mwanajeshi wa Marekani ambaye alijaribu kujichoma moto Jumapili mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington, kupinga vita vya Gaza, amefariki kutokana na majeraha yake, jeshi la Marekani limetangaza Jumatatu.

Waandamanaji wanaounga mkono Palestina wanakamatwa na polisi wa Mamlaka ya Bandari baada ya kuzuia usafiri kwenye barabara inayoelekea Uwanja wa Ndege wa John F Kennedy (JFK), mjini New York, Marekani, Desemba 27, 2023.
Waandamanaji wanaounga mkono Palestina wanakamatwa na polisi wa Mamlaka ya Bandari baada ya kuzuia usafiri kwenye barabara inayoelekea Uwanja wa Ndege wa John F Kennedy (JFK), mjini New York, Marekani, Desemba 27, 2023. REUTERS - STEPHANIE KEITH
Matangazo ya kibiashara

"Mtu aliyehusika katika tukio la jana alifariki jaan usiku kutokana na majeraha," Rose M. Riley, msemaji wa Pentagon, amesema katika ujumbe mfupi uliotumwa kwa shirika la habari la AFP.

"Tutatoa taarifa zaidi saa 24 baada ya ndugu kufahamishwa," ameongeza.

Idara ya Huduma za Dharura iliharakia kwenye eneo la tukio muda mfupi kabla ya saa saba mchana siku ya Jumapili kuitikia "wito kuhusu mtu aliyekua akiungua mbele ya ubalozi wa Israel," idara ya zima moto ya mji mkuu imesema kwenye X.

Walipofika, walikuta Secret Service, idara ya ulinzi ya maafisa wa ngazi za juu wa Marekani, tayari walikuwa wamezima moto.

Mwanamume huyo alipelekwa hospitalini akiwa na "majeraha mabaya na ya kutishia maisha," kulingana na chanzo kimoja.

Msemaji wa jeshi la wanahewa amethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba alikuwamawanjeshi, bila kutoa maelezo zaidi.

Kwa upande wake, ubalozi wa Israel ulisema kwamba hakuna wafanyakazi waliojeruhiwa wakati wa tukio hilo na kwamba mwanajeshi wa Marekani "hajulikani".

Video, iliyoonyeshwa moja kwa moja kwenye jukwaa la Twitch kulingana na ripoti za vyombo vya habari na kisha kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, inaonyesha mwanamume aliyevalia sare za kijeshi akijinyunyiza kioevu kabla ya kuimba "Palestina Huru!" (Ikomboe Palestina!) huku akishika moto haraka mbele ya lango la ubalozi, hadi anaanguka chini.

“Sitashiriki tena katika mauaji ya halaiki. Nitashiriki katika kitendo cha kupinga kilichokithiri,” anatangaza mtu huyu kwenye video hii, ambayo shirika la habari la AFP haikuweza kuthibitisha mara moja.

Kitendo hiki kinakuja wakati maandamano yanaongezeka nchini Marekani kupinga hujuma mbaya ya Israel huko Gaza, inayotekelezwa kwa zaidi ya miezi minne, na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa lililofanywa tarehe 7 Oktoba nchini Israel na makomando wa vuguvugu la Kiislamu la Palestina.Hamas.

Marekani ndiye mfadhili mkuu wa kidiplomasia na kijeshi wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.