Pata taarifa kuu

Argentina: Rais Javier Milei ataka kuzuia haki ya kuandamana

Nchini Argentina, Javier Milei ambaye ni mliberali wa hali ya juu na anayependwa na watu wengi alichukua wadhifa wa mkuu wa nchi chini ya wiki moja iliyopita. Tayari ametangaza hatua kali za kufufua uchumi na kupambana na mfumuko wa bei: kushuka kwa thamani kwa zaidi ya 50% ya peso, na kupunguza kuanzia mwezi wa Januari 2023 ruzuku ya usafiri na nishati.

Nchini Argentina, Javier Milei ambaye ni mliberali wa hali ya juu na anayependwa na watu wengi alichukua wadhifa wa mkuu wa nchi chini ya wiki moja iliyopita. Na tayari, hatua zake nyingi za mshtuko zinazua maswali kati ya raia wa Argentina.
Nchini Argentina, Javier Milei ambaye ni mliberali wa hali ya juu na anayependwa na watu wengi alichukua wadhifa wa mkuu wa nchi chini ya wiki moja iliyopita. Na tayari, hatua zake nyingi za mshtuko zinazua maswali kati ya raia wa Argentina. AFP - JUAN MABROMATA
Matangazo ya kibiashara

Na ili kuzuia maandamano ambayo hatua hizi zinaweza kuchochea, anapanga kufanya uingiliaji kati wa polisi dhidi ya mashirika na watu binafsi wanaoandamana, na vile vile vikwazo kwa wazazi wanaoenda kwenye maandamano na watoto wao.

Kuwatuma maafisi wa polisi kuwakabili wale wanaoingia barabarani au kuwachukulia vikwazo wazazi wanaoenda kwenye maandamano na watoto wao, Rais Javier Milei anazuia haki ya kuandamana. Brian Shapira, katibu wa zamani wa Haki za Kibinadamu katika serikali ya Rais wa zamani Maurico Macri, ambaye sasa ni mshirika wa Javier Milei, anaunga mkono msimamo wa rais Milei: "Waache waandamanaji wakabiliwe vilivyo na polisi, inaonekana hiyo inafaa kwangu. Lakini mjadala wa vizuizi vya barabarani unaonekana kuwa jambo la kawaida kwangu, kwa sababu ni tatizo ambalo linaathiri sana makumi au hata mamia ya maelfu ya wafanyakazi. "

"Kinyume cha katiba kabisa"

Lakini pia "kwa sababu usafiri mwingi wa umma hupita katika mitaa hii, na watu wengi hunyimwa haki zao za kwenda kazini," anahitimisha Brian Shapira. Vyama vya wafanyakazi vinapinga kabisa hoja hizo. Ricardo Peidro, naibu katibu wa muungano wa CTA Autonoma, anasema "ni kinyume cha katiba kabisa. Anataka kudumisha uaminifu wa sehemu ya wapiga kura wake, wanaokataa maandamano yoyote ya raia. Serikali hii mpya inakabiliwa na mfumo ambapo maskini wanawakilisha 40% ya raia. Inapaswa kukabiliana na kile kinachosababisha hali hii, na si kutumia vurugu kujibu madai ya waandamanaji. "

Mtihani wa kwanza wa kweli kwa hatua hizi: wakati wa maandamano ya wiki ijayo; wanaadhimisha mzozo wa kiuchumi wa mwaka 2001 na ukandamizaji mkali wa polisi ambao uliua watu 39 wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.