Pata taarifa kuu

Argentina : Javier Milei na Sergio Massa waelekea kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Nairobi – Raia wa Argentina wanatarajiwa kupiga kura tena mwezi ujao ili kumchagua Rais baada ya matokeo ya hapo jana jumapili na hivyo watalazimika kuchagua kati ya mgombea wa mrengo wa kushoto Sergio Massa na Javier Milei wa mrengo wa kulia.

Javier Milei na Sergio Massa waelekea kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwezi ujao
Javier Milei na Sergio Massa waelekea kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwezi ujao Β© @Reuters
Matangazo ya kibiashara

Huku kura nyingi zikiwa zimehesabiwa, hakuna mgombeaji aliyepata zaidi ya 45% ya kura naΒ  ambacho ni kiwango cha juu kinachobaini mshindi.

Matokeo hayo yamewashangaza raia wengi, ambao walidhani wapiga kura wangemwadhibu Bw Massa kwa kusimamia mgogoro mkubwa kama waziri wa uchumi wakati huu mfumuko wa bei nchini Argentina ukikaribia asilimia 140%.

Kulingana na matokeo ya hapo jana ni kuwa Bw MassaΒ  anaongoza baada yakupata 36.2% ya kura ilhali Bw Milei alipata 30.2% ya kura.Hapo awali Bw Milei alikuwa akiongoza.

Vyombo vya habari vya ndani vinaripotiΒ  kuwa takribani wapiga kura asilimia 74,walijitokeza kwenye shughuli hiyo .Argentina imeshuhudia kuongezeka kwa uungwaji mkono kwa Bw Milei ,mwenye siasa kali za mrengo wa kulia, ambaye ameapa kufuta benki kuu na kuchukua nafasi ya peso ya Argentina na dola ya Marekani.

Pamoja na kuahidi mabadiliko katika sera za kiuchumi, Bw Milei amefanya kampeni ya kupunguza afisi za serikali kwa kile anachosema kuwa kitapunguza urasimu serikalini.

Waziri wa sasa wa uchumi Bw Massa na waziri wa zamani wa usalama Patricia Bullrich walikuwa wapinzani wakuu wa Bw Milei kabla ya kura ya hapo jana.

Wawili hao ni washambuliaji Β wakubwa kutoka muungano wa jadi wa Argentina.Bw Massa alilenga sehemu kubwa ya kampeni yake katika kutetea sifa za kijamii na kazi za chama cha Peronist.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 51 alisisitiza kuwa hatua za kubana matumizi zilizopitishwa na serikali yake ni matokeo ya deni la IMF lililoendeshwa na utawala wa hapo awali wa mrengo wa kulia.

Idadi ndogo ya kura ilipendekeza kuwa 23.8% ya kura zilimwendea Bi Bullrich wa mrengo wa kulia, ambaye alikuwa ameahidi kurejesha "utaratibu" nchini. Alikuwa waziri wa usalama kati ya 2015 na 2019 wakati wa uongozi wa kati wa kulia wa Buenos Aires.

Wanaofuatia nyuma ya wagombea wote watatu walikuwa wanasiasa Juan Schiaretti na Myriam Bregman.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.