Pata taarifa kuu

Argentina: Mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia Javier Milei ashinda uchaguzi wa urais

Mwishoni mwa uchaguzi wa urais nchini Argentina siku ya Jumapili jioni, mgombea mwenye msimamo mkali zaidi Javier Milei alichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri kwa 55.95% ya kura, kulingana na matokeo rasmi ya sehemu ya kwanza. Mpinzani wake Sergio Massa, Waziri wa sasa wa Uchumi, alikubali kushindwa kwa 44.04% ya kura. Matokeo kati ya wagombea hao wawili, hata hivyo, yalionekana kukaribiana, huku nchi ikiwa imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Rais Mteule, kutoka muungano wa Liberty Advances, Javier Milei akipongeza ushindi wake baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais mjini Buenos Aires, Jumapili, Novemba 19, 2023.
Rais Mteule, kutoka muungano wa Liberty Advances, Javier Milei akipongeza ushindi wake baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais mjini Buenos Aires, Jumapili, Novemba 19, 2023. © Natacha Pisarenko / AP
Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo, yakionyesha kuongoza kwa zaidi ya pointi 11 kwa Javier Milei, yaliwasilishwa na sekretarieti ya kuu ofisi ya rais, huku zaidi ya asilimia 86 ya kura zikiwa zimehesabiwa. Dakika chache mapema, Sergio Massa alikubali kushindwa, akiwatangazia wafuasi wake kwamba Javier Milei "ndiye rais ambaye raia wengi wa Argentina wamemchagua kwa miaka minne ijayo". Ugombea wake ulilemewa na mzozo wa kiuchumi ambao haujawahi kutokea katika miaka 20 nchini humo.

Aliongeza kuwa alimpigia simu Javier Milei "ili kumpongeza na kumtakia mafanikio mema".

Wakati huo huo, furaha ilijaa nje ya makao makuu ya kampeni ya Javier Milei, ambapo maelfu ya wafuasi waliimba nyimbo mbili zinazopendwa na mgombea: "La caste tiene miedo" ("kundi linagopa!" ) "Viva la libertad, karajo!” » ("Uhuru uwepu kwa kipndi refu,!"). "Waende wote, asibaki hata mmoja!" ", pia alisisitiza wafuasi wa Milei, wakipeperusha bendera za manjano na picha ya simba - picha iliyokuzwa na Milei mwenyewe, ikitoa manyoya yake ya nywele.

"Tunakabiliwa na matatizo makubwa," anaonya Milei

Katika hotuba yake ya ushindi, Javier Milei alithibitisha kwamba "leo huanza mwisho wa uharibifu" na "ujenzi upya wa Argentina", lakini alionya kwamba hakutakuwa na "hatua nusu". "Huu ni usiku wa kihistoria kwa Argentina," Milei aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika makao makuu ya kampeni yake huko Buenos Aires. "Mfano duni wa tabaka umekwisha, leo tunachukua kielelezo cha uhuru, ili kuwa mamlaka ya ulimwengu tena," aliongeza. Leo inamaliza njia moja ya kufanya siasa, na inaanza nyingine."

"Tunakabiliwa na matatizo makubwa: mfumuko wa bei, vilio, ukosefu wa kazi halisi, ukosefu wa usalama, umaskini na taabu," aliorodhesha rais mteule. "Matatizo ambayo yatakuwa na suluhu tu ikiwa tutakumbatia tena mawazo ya uhuru."

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alimpongeza Javier Milei mwenye msimamo mkali siku ya Jumapili kwa kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Argentina kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, akisema "ataibadilisha" nchi yake. "Ninajivunia sana. Utaibadilisha nchi yako na kuifanya Argentina kuwa kubwa tena,” Bw. Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, kabla ya kuchapishwa kwa matokeo rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.