Pata taarifa kuu

BRICS yapokea wanachama sita wapya zikiwemo Misri na Ethiopia

BRICS (Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini), wanaokutana katika mkutano wa kilele mjini Johannesburg, watapokea wanachama sita wapya kuanzia mwezi Januari, ikiwa ni pamoja na Iran, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza siku ya Alhamisi.

Argentina, Misri, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinajiunga na BRICS (Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini).
Argentina, Misri, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinajiunga na BRICS (Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini). AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

Iran, Argentina, Misri, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinajiunga na kundi la nchi zinazoibukia zinazotaka kupata ushawishi duniani.

"Uanachama utaanza kutekelezwa kuanzia Januari 1, 2024," Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema katika mkutano wa pamoja wa viongozi wa mataifa matano ambayo kwa sasa yanaunda muungano huo. "Kwa mkutano huu wa kilele, BRICS inaanza na ukurasa mpya," amesema.

Siku moja kabla, Pretoria ilitangaza kuwa nchi zote wanachama zimekubaliana juu ya kanuni ya upanuzi.

"Tumepitisha waraka ambao unaweka miongozo, kanuni na taratibu za mapitio kwa nchi zinazotaka kuwa wanachama wa BRICS," alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor, akiangazia hatua 'chanya' iliyopigwa.

Baadhi ya nchi arobaini zilikuwa zimetuma maombi ya uanachama au zilionyesha nia ya kujiunga na BRICS. Kulingana na viongozi wa "kundi la nchi tano", ambalo linazalisha robo ya utajiri wa dunia na kuleta pamoja 42% ya idadi ya watu duniani, shauku hii inaonyesha kuongezeka kwa ushawishi wa nchi zinazoibuka duniani.

Majadiliano

Suala la upanuzi wa kundi lilikuwa kipaumbele cha mkutano huu wa 15 uliofunguliwa siku ya Jumanne. Muungano wa mataifa ya mbali kijiografia na uchumi wenye ukuaji usio sawa, BRICS ilibidi kukubaliana kuhusu chaguo la kimkakati la washiriki wapya.

Mazungumzo hayo yalifanyika wakati wa kikao cha mashauriano kilichofanyika kwa faragha siku ya Jumatano. Mikutano baina ya nchi mbili pia imeongezeka tangu kufunguliwa kwa mkutano huo.

BRICS ilithibitisha tena msimamo wao wa "kutofungamana na upande wowote" katika mkutano huo, wakati ambapo mgawanyiko umechochewa na mzozo nchini Ukraine. Marekani imesema haioni BRICSkama "wapinzani wa kijiografia" wa siku zijazo, ikisema inataka kudumisha "uhusiano thabiti" na Brazil, India na Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.