Pata taarifa kuu

Haiti: Kikosi cha kimataifa kutumwa, lakini hakina kasi ya kutosha kwa serikali ya mpito

Baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo, jeshi la polisi la kimataifa kusaidia Haiti, inayokabiliwa na ghasia za magenge, linaanza kuchukua sura, lakini kwa mwendo wa kinyonga kulingana na Waziri Mkuu ambaye kwa mara nyingine ameutaka Umoja wa Mataifa "kuchukua hatua", haraka.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Nganga Mutua (kulia), Septemba 22, 2023 mjini New York.
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Nganga Mutua (kulia), Septemba 22, 2023 mjini New York. AP - Bing Guan
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa, Septemba 22, Marekani ilitangaza kwamba nchi kadhaa zilikusudia kuchangia chini ya uongozi wa Kenya kwa kikosi hiki ambacho Haiti imekuwa ikiomba kwa mwaka mmoja, lakini bila shaka uanzishwaji wake utachukua miezi michache zaidi, bila kusahau idadi ya kikosi hiki.

"Raia wa Haiti wanakabiliwa kila kukicha na masha magumu, ndiyo maana Baraza la Usalama (...) linapaswa kuchukuwa hatua za haraka kwa kuidhinisha kutumwa kwa ujumbe wa kimataifa wa usaidizi wa usalama, polisi na jeshi," aliomba Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry siku ya Ijumaa mbele ya jukwaa la Umoja wa Mataifa, huku kura ikitarajiwa kupigwa hivi karibuni, labda wiki ijayo.

"Ninaomba jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua, na kuchukua hatua haraka," alisisitiza, akiorodhesha mambo ya kutisha ambayo magenge yanatendea raia wake. "Utekaji nyara kwa ajili ya fidia, uporaji, visa vya uchomaji moto, mauaji ya hivi karibuni, unyanyasaji wa kijinsia, biashara haramu ya binadamu, mauaji, mauaji nje ya watu wanaoshikiliwa na vyomvo vya dola, kuajiri watoto askari, kufunga barabara kuu," alisema.

Wito kwa Wahaiti

Ariel Henry pia alitoa wito kwa Wahaiti kushiriki katika mazungumzo haya ambayo kwa sasa hayana mkwamo. "Kwa mara nyingine tena, kutoka juu ya jukwaa hili, natoa wito kwa Wahaiti wote wenye nia njema, wale wanaoishi katika nje ya nchi, pamoja na wale wa ndani, wadau wote katika siasa  nchini Haiti, bila kujali sera zao, kufanya kazi na serikali kupambana dhidi ya magenge haya, kurejesha usalama na kama wanademokrasia wa kweli, kuchukua mamlaka kupitia sanduku la kura, alisema. Serikali hii ya mpito ninayoiongoza imedhamiria kufanya uchaguzi haraka iwezekanavyo. Na katika siku zijazo, licha ya hali inayojiri, nitakamilisha, kwa makubaliano na Baraza Kuu la Mpito, hatua za kuzindua mchakato wa uchaguzi, kwa kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.”

Nchi kumi hadi kumi na mbili zinaweza kuhusika

Magenge hayo, ambayo yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu wa nchi hii maskini ya Karibea na kueneza utawala wa ugaidi, yameua zaidi ya watu 2,400 tangu kuanza kwa mwaka huu, kulingana na Umoja wa Mataifa. Polisi wa kitaifa wa Haiti, hata hivyo, hawawezi kukabiliana nao, kwa hivyo wazo la jeshi la kimataifa kusaidia nchi hii ambayo inakabiliwa na migogoro mingi ya kisiasa na kibinadamu.

"Kutoka nchi 10 hadi 12 zimeombwa kujiunga na ujumbe huu" wa msaada wa usalama kwa polisi huko Haiti, ambaini naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Victoria Nuland, baada ya mkutano wa mawaziri huko Haiti kando ya Mkutano Mkuu.

Alikataa kutaja nchi hizo, lakini Jamaica, Bahamas na Antigua na Barbuda zimeonyesha kuwa zitashiriki. Kenya, ambayo ilijitolea kuongoza kikosi hicho, ilijitolea kutoa wanajeshi 1,000 wa kikosi cha usalama. Marekani inakusudia kutoa usaidizi mkubwa wa vifaa (usafiri wa anga, mawasiliano, makazi, matibabu) lakini si vikosi vya usalama wa ardhini kuwa kipaumbele.

'Hakuna muda wa kupoteza'

"Ujumbe huu wa usaidizi hautachukua nafasi ya maendeleo katika ngazi ya kisiasa," alisema mkuu wa diplomasia ya Marekani, Antony Blinken, wakati wa mkutano huo, akisema anatumai kwamba kikosi hiki kinaweza "kutumwa ndani ya miezi michache" kwa sababu "hakuna muda wa kupoteza”.

Waziri wa Mambo ya Nje pia alitangaza kuwa serikali ya Joe Biden itaomba Bunge la Congress dola milioni 100 ili kufadhili shuguli hiyo. Hii lazima iwe na sehemu muhimu ya polisi lakini pia sehemu ya kijeshi katika kuunga mkono polisi wa Haiti. Dhamira yake ni kutoa msaada wa kiutendaji kwa polisi, kuhakikisha usalama wa mitambo muhimu na barabara na kuimarisha polisi kwa muda mrefu.

Kikosi kisio kuwa cha Umoja wa Mataifa

Kikosi hiki kinasubiri idhini kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuanzishwa, hata kama haitafanywa chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Waziri Mkuu wa Barbados, Mia Mottley, amesema "ni matumaini kwamba wajumbe wa Baraza la Usalama watakubali kwamba hawawezi kutumia Haiti kama mpira, kwa sababu (Wahaiti) wameteseka kwa muda mrefu sana, kati ya mikono ya nchi nyingi sana." , bila kutoa maelezo zaidi. Rasimu ya azimio iliyoandaliwa na Marekani na Ecuador itajadiliwa wiki ijayo katika Umoja wa Mataifa, alisema Victoria Nuland, akionyesha "uungaji mkono mkubwa" kwa nakala hii.

Katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, Rais wa Marekani Joe Biden alitoa wito kwa Baraza la Usalama "kuidhinisha sasa" kutumwa kwa jeshi la kimataifa nchini Haiti kwa sababu "watu wa Haiti hawawezi kusubiri tena".

Mwenzake wa Kenya William Ruto alifanya vivyo hivyo siku ya Alhamisi, akiona kuwa "haitokubalika" kuwatenga watu wa Haiti. Kwa takriban mwaka mzima, Ariel Henry, amekuwa akitoa wito wa kutumwa kwa kikosi kama hicho.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.