Pata taarifa kuu

Rekodi za ubakaji nchini Brazil mnamo 2022, zaidi ya nane kwa saa

Brazil ilikumbwa na mlipuko wa unyanyasaji wa kijinsia mnamo 2022, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya kongamano la usalama wa umma iliyochapishwa siku ya Alhamisi. Licha ya kupungua kidogo kwa vifo vya kikatili, rpoti hii inabaini hali ya kutisha, idadi ya ubakaji uliorekodiwa nchini haijawahi kuwa kubwa kama mwaka jana. Takriban waathiriwa 75,000 kwa jumla. Ongezeko la ukatili wa kijinsia unaowahusu wanawake, lakini pia watoto.

Maandamano wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake nchini Brazili, Machi 8.
Maandamano wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake nchini Brazili, Machi 8. AFP - MIGUEL SCHINCARIOL
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini Brazili, Théo Conscience

"Katika ukatili dhidi ya watoto na vijana, itakuwa vigumu kuwasilisha hali mbaya zaidi kuliko ile ya mwaka 2022", wanaandika waandishi wa ripoti hiyo. Unyanyasaji, ponografia ya watoto, unyanyasaji wa kingono… Viashiria vyote vinaongezeka na vingine vimekithiri kwa kuaongezeka, kama vile idadi ya ubakaji wa watoto, ambayo imeongezeka kwa zaidi ya 15%.

Wakati wa kutafuta sababu za ongezeko hili, ripoti inaendeleza jukumu ambalo janga la Uviko-19 linaweza kuwa limechukua na hasa kufungwa kwa shule ambazo kulifanya watoto kuwa katika hatari ya kushambuliwa nyumbani mwao, huku ikiwanyima msaada ambao mazingira ya shule hutoa mara nyingi.

Zaidi ya theluthi mbili ya ubakaji (68.3%) ulifanywa katika nyumba za waathiriwa. Na idadi kubwa ya waathiriwa wenye umri wa miaka 0 hadi 13 walibakwa na watu wanaowafahamu (86.1%) au watu wa familia zao (64.4%).

Wahanga wengine wakubwa wa mlipuko huu wa ukatili ni wanawake. Idadi ya wanawake kuuawa imeongezeka kwa 6%. Na waathiriwa 9 kati ya 10 wa ubakaji ni wanawake. Huku kukiwa na takriban malalamiko 75,000 yaliyorekodiwa mwaka jana, idadi ya ubakaji imefikia rekodi ya kihistoria, jambo la kutisha zaidi ikizingatiwa kwamba kulingana na utafiti wa IPEA, ni asilimia 8 tu ya ubakaji ulioripotiwa kwa polisi nchini Brazil. Kulingana na takwimu hii, ripoti inakadiria kuwa jumla ya idadi ya ubakaji katika kipindi cha mwaka 2022 inaweza kuwa karibu 822,000.

Ripoti ya shirika moja lisilo la kiserikali pia imebainisha mauaji ya wanawake 1,437 , ongezeko la 6.1% ikilinganishwa na mwaka uliopita, na kesi 245,713 za unyanyasaji wa majumbani (ongezeko la 2.9%).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.