Pata taarifa kuu

Rais wa Brazil Lula awasili mjini Brussels kwa ajili ya mkutano wa kilele wa CELAC-EU

Viongozi wa Amerika Kusini wanaanza kuwasili Brussels Jumapili hii, Julai 16, kwa mkutano kati ya Jumuiya ya Amerika ya Kusini na Caribbean (CELAC) na Umoja wa Ulaya, unaoanza Jumatatu. Miongoni mwa Viongozi thelathini wa Nchi zinazovuka Atlantiki, Lula anatarajiwa hasa. Atajaribu, miongoni mwa mambo mengine, kufanya maendeleo kwenye mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na MERCOSUR (Argentina, Brazil, Paraguay na Uruguay).

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen mjini Brasilia Juni 12, 2023.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen mjini Brasilia Juni 12, 2023. AP - Gustavo Moreno
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyombo vya habari vya Brazil, kuna uwezekano mdogo kwamba mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria yataendelea wakati wa mkutano huu. Kwa hakika, mkutano kati ya rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, na Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, umepangwa kufanyika. Lakini maungumzo yao yatakuwa ya ishara tu.

Brazil imemaliza kuandika barua ambayo imekusudiwa kujibu mahitaji ya mazingira ya Ulaya. Barua hiyo itawasilishwa kwanza kwa washirika wa MERCOSUR kabla ya kutumwa kwa Umoja wa Ulaya. Hali ambayo itachukua wiki chache zaidi, kulingana na vyanzo kutoka Brazil.

Kuimarisha uhusiano kati ya nchi za Ulaya na Amerika ya Kusini

Hii ndiyo sababu mkutano huo unapaswa kuzingatia kuimarisha uhusiano kati ya nchi za Ulaya na Amerika Kusini. Lula anatarajia kuchukua jukumu muhimu katika mkutano huo. Kurejea madarakani kwa rais wa Brazil kumetoa msukumo mpya kwa Jumuiya ya Amerika ya Kusini na Caribbean, CELAC.

Katika mkutano wa Brussels, Lula pia anataka kushughulikia hali ya Nicaragua. Hivi majuzi kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis alimtaka aingilie kati kwa rais Daniel Ortega, ili kiongozi huyo awaachilie viongozi wa kidini waliokamatwa na mamlaka yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.