Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Rais wa zamani Bolsonaro ashtakiwa Brazil, mustakabali wake wa kisiasa mashakani

Miezi sita baada ya kuondoka madarakani, anakabiliwa na mashitaka: kumefunguliwa siku ya Alhamisi kesi ya rais wa zamani wa mrengo wa kulia wa Brazil Jair Bolsonaro, ambayo inaweza kumnyima kutekekeza haki zake za kisiasa na kumfanya asiwanii katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2026.

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro akilakiwa na wafuasi wake baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Porto Alegre, Brazili, Alhamisi, Juni 22, 2023.
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro akilakiwa na wafuasi wake baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Porto Alegre, Brazili, Alhamisi, Juni 22, 2023. © AP - Wesley Santo
Matangazo ya kibiashara

Wakati mustakabali wake wa kisiasa uko mikononi mwa majaji saba waliokusanyika katika maje,go rasmi ya Mahakama ya Juu ya Uchaguzi (TSE) huko Brasilia, Bw. Bolsonaro alikwepa mkutano huu ili kwenda Porto Alegre. Katika jiji hili kubwa la kusini, wafuasi kadhaa walimshangilia alipowasili kwenye uwanja wa ndege kabla ya mkutano ulioratibiwa na Chama chake cha Liberal, shirika la habari la AFP limebaini.

Mkuu huyo wa zamani wa nchi (2019-2022), ambaye anadai kuwa hana hatia, anashitakiwa kwa kushambulia mahakama ya uchaguzi na kukosoa, bila uthibitisho, uaminifu wa upigaji kura wa kielektroniki, miezi michache kabla ya uchaguzi alioshinda mpinzani wake wa mreno wa kushoto Luiz Inacio Lula da Silva.

Kulingana na hati ya mashtaka iliyosomwa wakati wa ufunguzi wa kikao cha TSE na jaji Benedito Goncalves, rais huyo wa zamani anashutumiwa kwa kutaka "kudhalilisha matokeo ya uchaguzi ya siku za usoni mbele ya jumuiya ya kimataifa, hadi wakati ambapo uchunguzi umeonyesha kuwa mpinzani wake ana nafasi nzuri ya kushinda".

Katika hotuba yake mnamo mwezi Julai 2022 katika makao ya rais ya Alvorada, na kutangazwa kwenye televisheni ya umma, Bw. Bolsonaro alitangaza mbele ya wanadiplomasia kwamba alitaka "kusahihisha dosari" katika upigaji kura wa kielektroniki kwa "ushiriki wa vikosi vya jeshi", bila kutoa ushahidi wowote wa tuhuma zake.

Upande wa mashtaka unamfungulia mashtaka kwa "matumizi mabaya ya mamlaka ya kisiasa na matumizi mabaya ya njia za mawasiliano".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.