Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA

Viongozi wa dunia walaani hatua ya wafuasi wa Bolsonaro kuvamia bunge

Viongozi mbalimbali  wa dunia wameenndelea kulaani hatua ya wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro kuvamia bunge, mahakama na Ikulu siku ya Jumapili.

Wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro walipovamia bunge
Wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro walipovamia bunge AP - Eraldo Peres
Matangazo ya kibiashara

China imesema inakashifu vikali kitendo hicho, Msemaji wa wizara ya wa mambo ya kigeni ya China Wang Wenbin ameleza  taifa lake linaunga mkono hatua ambazo serikali ya Brazil imechukua kurejesha utulivu.

Kinara wa upinzani nchini Kenya, mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, naye pia ameelani kitendo hicho anachosema ni tishio na aibu kwa demokrasia na asasi huru za kidemokrasia.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa upande amesema nchi yake inasimama na rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.

Scholz, amesisitiza kuwa mashambulio katika asasi huru za kidemokrasia hayakubaliki.

Rais Luiz Inacio Lula da Silva ametangaza kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali watu wote waliohusika na kupanga njama hiyo ya kushambulia majengo ya serikali katika taifa lake.

Wafuasi wa rais wa zamani Jair Bolsonaro wamekataa kukubali kuwa mgombea wao alishindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.