Pata taarifa kuu

Uvamizi wa majengo ya serikali: Jair Bolsonaro ahusishwa akiwa ugenini

Aliyekuwa rais wa Brazil Jair Bolosonaro alikuwa nje ya nchi huko Floride, nchini Marekani, maelfu ya kilomita kutoka nchi yake, wakati wafuasi wake wakivamia majengo ya serikali nchini Brazil. Hata hivyo ameendelea kukabiliwa na lawama kutoka kambi ya rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva.

Msafara wa Jair Bolsonaro ulipowasili Orlando, Florida, Desemba 30, 2022.
Msafara wa Jair Bolsonaro ulipowasili Orlando, Florida, Desemba 30, 2022. REUTERS - OCTAVIO JONES
Matangazo ya kibiashara

Jair Bolsonaro aliwasili Florida mnamo Desemba 30, kwa wakati unaofaa ili kutohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa mrithi wake Luiz Inacio Lula da Silva. Rais wa zamani wa Brazil amepata hifadhi katika mji wa Orlando, katika jombo la Frorida, nchini Maekani.

Anakaa maili chache kutoka kwenye bustani ya mandhari ya Disney World, katika nyumba ya kukodisha inayomilikiwa na mfuasi wa muda mrefu, Jose Aldo, raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 36, bingwa wa zamani wa MMA(mchanganyiko wa Sanaa ya Vita). Bolsonaro anapanga kukaa huko hadi mwishoni mwa mwezi wa Januari.

Wito wa kufukuzwa

Kwenye mitandao, video zinaonyesha rais huyo wa zamani akiwa amevalia kaptula na fulana akiwasalimia wafuasi wachache katika mitaa ya kitongoji cha watu matajiri. Katika video zingine, Bolsonaro ameweza kuonekana akiishi maisha ya mkaazi mmoja wa Florida wa kawaida, akinunua kuu katika duka kubwa.

Lakini wakati vituo vya habari vya Marekani vikitangaza picha za moja kwa moja za wafuasi wake wakivamia maeneo ya mamlaka nchini Brazil, kwenye Twitter baadhi ya wabunge wa chama cha Democratic walimtaka Gavana wa Republican wa jimbo la Florida Ron DeSantis kumfukuza rais huyo wa zamani wa Brazil.

Viongozi mbalimbali  wa dunia walaani hatua ya wafuasi wa Jair 

China imesema inakashifu vikali kitendo hicho, Msemaji wa wizara ya wa mambo ya kigeni ya China Wang Wenbin ameleza  taifa lake linaunga mkono hatua ambazo serikali ya Brazil imechukua kurejesha utulivu.

Kinara wa upinzani nchini Kenya, mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, naye pia ameelani kitendo hicho anachosema ni tishio na aibu kwa demokrasia na asasi huru za kidemokrasia.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa upande amesema nchi yake inasimama na rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.

Scholz, amesisitiza kuwa mashambulio katika asasi huru za kidemokrasia hayakubaliki.

Rais Luiz Inacio Lula da Silva ametangaza kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali watu wote waliohusika na kupanga njama hiyo ya kushambulia majengo ya serikali katika taifa lake.

Wafuasi wa rais wa zamani Jair Bolsonaro wamekataa kukubali kuwa mgombea wao alishindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.