Pata taarifa kuu

Rais wa zamani wa Brazil Bolsonaro aomba visa mpya ya miezi sita ili kusalia Marekani

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, ambaye anachunguzwa kwa jukumu lake katika shambulio la ghasia kwenye makao makuu ya taasisi za kitaifa huko Brasilia mnamo Januari 8, ametuma maombi ya visa ya miezi sita ya kusalia nchini Marekani, wakili wake alisema siku ya Jumatatu Januari 30.

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, ambaye anachunguzwa kwa jukumu lake katika shambulio la ghasia kwenye makao makuu ya taasisi za kitaifa huko Brasilia mnamo Januari 8, ametuma maombi ya visa ya miezi sita ya kubaki Marekani.
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, ambaye anachunguzwa kwa jukumu lake katika shambulio la ghasia kwenye makao makuu ya taasisi za kitaifa huko Brasilia mnamo Januari 8, ametuma maombi ya visa ya miezi sita ya kubaki Marekani. AP - Bruna Prado
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani wa mrengo wa kulia aliondoka Brazil na kuelekea Florida siku mbili kabla ya kuapishwa kwa Lula mnamo Januari 1, na visa yake ya sasa inatazamiwa kuisha hivi karibuni, kulingana na ofisi ya mawakili ya AG Immigration.

Bw. Bolsonaro anasemekana kuingia Marekani kwa visa iliyotolewa kwa viongozi walio ziarani, ambayo inaisha siku ya Jumanne kwa kuwa hafanyi kazi tena rasmi. Ilipoulizwa kuhusu ombi la visa la Jair Bolsonaro, wizara ya mambo ya Nje imejibu kwamba aina hii ya habari ni ya siri nchini Marekani.

Rais huyo wa zamani wa Brazil alisema kwene kituo cha habari cha CNN nchini Brazil kwamba alipanga kurejea nchini Brazil mwishoni mwa mwezi Januari na kwamba alikuwa anafikiria kurudi nchini Marekani kwa sababu za kiafya. Jair Bolsonaro alichomwa kisu mnamo 2018 alipokuwa akisafiri kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi. Tangu wakati huo amefanyiwa upasuaji mara kadhaa kwa ajili ya kuziba matumbo.

Wanademokrasia wenye hasira

Mnamo Januari 8, maelfu ya wafuasi wa Bolsonaro, ambao hawakufurahishwa na ushindi wa Lula da Silva dhidi ya rais wa zamani wa mrengo wa kulia katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba 2022, walivamia na kuharibu ikulu ya rais, mamakao makuu ya Bunge na Mahakama ya Juu zaidi huko Brasilia.

Siku chache baadaye, Wademokrat waliochaguliwa walimtaka Joe Biden kubatilisha visa ya Jair Bolsonaro, wakikataa kuwa Marekani ni kumpa hifadhi ya ukimbizi kiongozi huyo wa zamani. Anderson Torres, Waziri wa zamani wa Sheria anayemuunga mkono  Bolsonaro, alikamatwa mnamo Januari 14 kama sehemu ya uchunguzi wa ghasia hizo, wakati akirudi kwa ndege kutoka Marekani.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.