Pata taarifa kuu

Brazil: Watu 14 wafariki baada ya kuangukiwa jengo la ghorofa katika mji wa Recife

Watu kumi na wanne, wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na Jengo moja la katika mji wa Recife kaskazini-mashariki mwa Brazil kulingana na taarifa za waokoaji.

Waokoaji wakijaribu kutafuta manusura baada ya kuporomoka kwa jengo lililokaliwa kinyume cha sheria huko Paulista, karibu na Recife kaskazini-mashariki mwa Brazili, Julai 7, 2023.
Waokoaji wakijaribu kutafuta manusura baada ya kuporomoka kwa jengo lililokaliwa kinyume cha sheria huko Paulista, karibu na Recife kaskazini-mashariki mwa Brazili, Julai 7, 2023. © Alexandre AROEIRA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa watu watatu waliokolewa kwenye kifusi na wengine sita bado hawajulikani walipo, na utafutaji unaendelea.

Mkasa huu uliotokeasiku ya Ijumaa unakuja wakati Recife imekumbwa na mvua kubwa katika siku za hivi majuzi.

Watoto wawili, wenye umri wa miaka mitano na minane, walikuwa miongoni mwa waliofariki katika tukio hilo. Chanzo chamkasa huo hakijafahamika, lakini inashukiwa kua huenda umesababishwa na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika siku za hivi majuzi katiak mji wa Recife.

Kulingana na vyanzo kadhaa jengo hilo ni miongoni mwa majengo yenye mashaka ya usalama.

Wakati huo huo mamlaka katika eneo hilo imesema mvua zitaendelea kunyesha na kuwataka wakazi kuhammia katika maeneo yenye uhakika wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.