Pata taarifa kuu

White House ilitahadharishwa kuhusu uasi wa Wagner nchini Urusi

Mamluki wa kundi la Wagner wanaendelea kurudi kambini kusini mwa Urusi baada ya kundi hili la wanamgambo kujaribu kupindua kamandi ya jeshi la Urusi. Uasi uliosababishwa na mvutano kati ya mkuu wa Wagner na uongozi wa jeshi. Ishara za tahadhari ziligunduliwa na idara za ujasusi za Marekani katika miezi ya hivi karibuni.

Yevgeny Prigozhin, katika video iliyorekodiwa kutoka kwa akaunti ya Telegram ya Concord, idara ya vyombo vya habari yenye mafungamano na kundi la kijeshi cha Wagner.
Yevgeny Prigozhin, katika video iliyorekodiwa kutoka kwa akaunti ya Telegram ya Concord, idara ya vyombo vya habari yenye mafungamano na kundi la kijeshi cha Wagner. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Yevgeny Prigozhin ambaye anatayarisha hatua za kijeshi dhidi ya uongozi wa jeshi la Urusi: habari hiyo ilichukuliwa kuwa ya kuaminika na ya kutatanisha na idara za kijasusi huko Washington.

Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, kufikia siku ya Jumatano, Ikulu ya White House na baadhi ya wajumbe wa Congress walikuwa wamefahamishwa na idara za kijasusi kuhusu nia ya mkuu wa Wagner baada ya miezi kadhaa ya kazi. "Kulikuwa na ishara za kutosha kuweza kuwaambia viongozi kuna kitu kibaya," afisa wa Marekani ambaye hakutajwa jina ameliambia Gazeti la Washington Post. Marekani ilitaja, mnamo mwezi Januari, mvutano kati ya kundi la wanamgambo la Waner na Moscow.

Wasiwasi juu ya silaha za nyuklia za Urusi

Mvutano uliosababishwa na chuki kati ya Yevgeny Prigozhin, Sergei Choïgou na Valeri Guerassimov. Kwa miezi kadhaa, zaidi ya hayo, mkuu wa Wagner aliendelea kumkosoa Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi wa Urusi akiwashutumu kwa kutokuwa na uwezo katika usimamizi wao wa vita nchini Ukraine. Kwa upande wake, Sergei Shoigu alikuwa ameshinikiza kundi la Wagner liwekwe chini ya udhibiti wake.

Kulingana na gazeti hili la Marekani, mashirika ya kijasusi ya Marekani yalifahamishwa kuhusu hatua inayoweza kuchukuliwa na mkuu wa wanamgambo wa Wagner mapema katikati ya mwezi wa Juni. Kilichoshangaza mashirika ya upelelezi ya Marekani ni kasi ya hatua iliyofanywa na Yevgeny Prigozhin na wapiganaji wake. Wasiwasi wa maafisa wa Marekani ulihusu hasa matokeo ya uwezekano wa kuyumbishwa kwa Vladimir Putin na kushika udhibiti wa silaha za nyuklia za Urusi.

Kulingana na Gazeti la Marekani la Washington Post, Juni 10 ilikuwa muhimu katika uamuzi wa Prigozhin kukabiliana dhidi ya uongozi wa jeshi la Urusi. Siku hiyo, Wizara ya Ulinzi iliamuru mamluki wa Wagner kutia saini mikataba na jeshi, ambayo ilimkasirisha Yevgeny Prigozhin. Je, uasi huu utagharimu Sergei Shoigu na Valeri Guerassimov kazi zao? Hili ni moja ya maswali mengi ambayo wengi wanajiuliza kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.