Pata taarifa kuu

[Moja kwa moja] Uasi wa Wagner: Wakazi wa mkoa wa Lipetsk wahimizwa kubaki nyumbani

Baada ya kuchukua udhibiti wa Rostov-on-Don, kusini mwa Urusi, kundi la wanamgambo la Wagner linaelekea Moscow Jumamosi hii alasiri.

Msafara wa magari ya kijeshi ya kundi la mamluki la Wagner ukipita kwenye barabara kuu ya M-4, ambayo inaunganisha mji mkuu wa Urusi na miji ya kusini mwa Urusi, karibu na Voronezh, mnamo Juni 24, 2023.
Msafara wa magari ya kijeshi ya kundi la mamluki la Wagner ukipita kwenye barabara kuu ya M-4, ambayo inaunganisha mji mkuu wa Urusi na miji ya kusini mwa Urusi, karibu na Voronezh, mnamo Juni 24, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Unachopaswa kufahamu:

• Katika mfululizo wa jumbe za sauti, kiongozi wa Kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin ametoa wito wa uasi dhidi ya uongozi wa jeshi la Urusi. Anashutumu jeshi kwa kushambulia kambi za kijeshi za kundi la Wagner. Akidai kuongoza "maandamano ya kutafuta haki" na sio "mapinduzi ya kijeshi", Yevgeny Prigozhin anasema "yuko tayari kufa" na wapiganaji wake 25,000 kwa minajili ya "kuwakomboa raia wa Urusi".

• Gavana wa jimbo la Voronezh ameripoti mapigano ya wanajeshi wa Urusi. Mapema asubuhi, kiongozi wa Wagner alitangaza kwamba vikosi vyake vilivyowekwa nchini Ukraine hadi sasa vimevuka mpaka na kuingia Rostov, yalipo makao makuu ya kamandi ya kusini ya jeshi la Urusi, ambapo shughuli za kijeshi nchini Ukraine zinaratibiwa.

• Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi imetangaza kufunguliwa kwa uchunguzi kuhusu "uasi wa kutumia silaha" dhidi ya Yevgeny Prigozhin.

• Katika hotuba kwa taifa, Rais Vladimir Putin ameahidi hataruhusu "vita vya wenyewe kwa wenyewe" kutokea na kutoa wito wa "umoja". Akiuita uasi wa Wagner kuwa "tishio kuu", amemshutumu Yevgeny Prigozhin kwa "kusaliti" Urusi kwa sababu ya "matamanio yake mengi".

Wapiganaji wa Wagner katika eneo la Lipetsk

Gavana wa mkoa wa Lipetsk, karibu kilomita 400 kusini mwa Moscow, amebaini kwenye Telegram kwamba wapiganaji wa kundi la wanamgambo na Wagner "wanaelekea" makao makuu ya mkoa, hali amayo inathibitisha kusonga mbele kwa kundi hili kuelekea mji mkuu wa Urusi. "Vikosi vya usalama na mamlaka (...) vinachukua hatua zote muhimu ili kuhakikisha usalama wa raia. Hali imedhibitiwa, "anasema Igor Artamonov.

Ikulu ya Kremlin inasema inaungwa mkono na Rais wa Uturuki Erdogan

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, ofisi ya rais wa Urusi imebaini kwamba Vladimir Putin amepata "uungwaji mkono kamili" wa mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa mahojiano ya simu kuhusu kuzuka kwa uasi wenye silaha wa kundi la Wagner.

Ramzan Kadyrov kutuma wanajeshi wake kwenye 'maeneo ya mvutano'

"Wapiganaji kutoka Wizara ya Ulinzi na Walinzi wa Kitaifa wa Chechenya wanaelekea katika maeneo ya mvutano. Tutafanya kila kitu kulinda umoja wa Urusi na kulinda serikali yake,” Rais wa Chechnya Ramzan Kadyrov, ambaye wanajeshi wake walikuwa wakifanya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, amesema kwenye Telegram.

Hayo yanajiri wakati Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell amebaini kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa G7 walikutana kwa "kubadilishana mawazo". Hakuna maelezo yaliyochujwa kwenye maudhui ya mazungumzo hayo. Washington imebaini tu kwamba Marekani itasalia katika "uratibu wa karibu" na washirika wake baada ya mazungumzo haya ya kwanza, huku ikibainisha kuwa uasi huu hautabadilisha chochote katika kuunga mkono Ukraine.

Uasi nchini Urusi, ni 'fursa' kwa Ukraine

Urusi imeanza mchakato unaopelekea uharibifu wake yenyewe kwa kuivamia Ukraine, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Ganna Maliar amesema kwenye Telegram. “Hii ina maana gani kwetu? Kuzuka kwa uasi uu utatupa dirisha la fursa", ameongeza, akihakikisha kwamba Ukraine inaendelea na kazi yake ya "ushindi".

Yevgeny Prigozhin anadai kuchukua makao makuu ya kijeshi ya Rostov 'bila mapigano

“Kwa nini nchi inatuunga mkono? Kwa sababu tunaandamana kutafuta haki,” amesema mkuu wa Wagner, anayeshutumiwa kwa "uhaini" na Vladimir Putin, katika ujumbe wa sauti kwenye Telegram. "Tuliingia Rostov, na bila kufyatua risasi hata moja, tulichukua jengo la makao makuu," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.