Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky: Udhaifu wa Urusi unaonekana 'dhahiri'

Katika kauli yake ya kwanza kwa matukio ya Urusi, rais wa Ukraine anaona kwamba uasi wa kundi la Wagner unaonyesha udhaifu wa "jumla" wa Urusi, iliotumbukia katika "uovu na machafuko". Yeyote "anayechagua njia ya uovu anajiangamiza mwenyewe", anasema Volodymyr Zelensky, akibaini mtazamo wa Vladimir Putin ambaye "hutuma mamia ya maelfu ya watu vitani ili kujizuia katika mkoa wa Moscow ili kujilinda dhidi ya wale ambao yeye mwenyewe amewapa silaha. ”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, wa pili kulia, akimsikiliza kamanda wa kijeshi alipotembelea eneo la Donetsk, Ukraine, Jumanne, Mei 23, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, wa pili kulia, akimsikiliza kamanda wa kijeshi alipotembelea eneo la Donetsk, Ukraine, Jumanne, Mei 23, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

“Jaribio lolote la kuanzisha mifarakano nchini ni uhalifu mkubwa zaidi ambao hauwezi kuungwa mkono wala kutoa nafasi ya kujitetea,” amesema kiongozi wa Kanisa la Othodoksi nchini Urusi na mshirika wa Rais Vladimir Putin. "Ninatoa wito kwa wale waliochukua silaha kuwaelekeza dhidi ya ndugu zao kufikiria upya" chaguo lao, ameongeza, akisema "kuunga mkono juhudi za Vladimir Putin kuzuia machafuko" nchini Urusi.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel anasema "anafuatilia kwa karibu hali ya Urusi" na "kuwasiliana na viongozi wa Ulaya na washirika wa G7", baada ya kundi la Wagner kuingia katika uasi. "Hili ni tatizo la ndani ya Urusi. Usaidizi wetu kwa Ukraine na Volodymyr Zelensky hautetereki,” ameongeza afisa huyo wa Ulaya.

Katika mahojiano na BBC, mkuu wa serikali ya Uingereza Rishi Sunak anatoa wito kwa upande wake "wahusika wote kuwajibika na kulinda raia". Kwa upande wa Rais wa Baraza la Italia Giorgia Meloni, matukio haya "yanaonyesha jinsi uchokozi dhidi ya Ukraine pia unavyosababisha kukosekana kwa utulivu" nchini Urusi. Katika mtandao wa Twitter, Waziri wake wa Mambo ya Nje Antonio Tajani anatoa wito kwa raia wa Italia nchini Urusi kuwa makini.

Yevgeny Prigozhin abaini kwamba Vladimir Putin 'ana makosa makubwa'

Akijibu hotuba ya rais wa Urusi, kiongozi wa kundi la Wagner anathibitisha katika rekodi ya sauti kwamba mkuu wa Kremlin "ana makosa makubwa" kwa kuwashutumu wapiganaji wake kwa "uhaini". "Sisi ni wazalendo", ametangaza Yevgeny Prigozhin, akihakikisha kwamba askari wake hawana nia ya "kujisalimisha".

Sisi ni wazalendo. Na wanaotupinga leo ni wale waliojikusanya kuzunguka majungu.

Wakati huo huo Wakuu wa mabaraza mawili ya Bunge la Urusi wametoa wito wa kumuunga mkono Vladimir Putin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.