Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Hali ya wasiwasi yatanda Moscow, Putin hajulikani aliko

Kiongozi wa kundi la wanamgambo Wagner Yevgeny Prigozhin ameapa Jumamosi kwenda "hadi mwisho" kupindua kamandi ya jeshi la Urusi, ambayo anaituhumu kwa kuwalipua watu wake kwa mabomu, upande wa mashtaka ukitangaza kwa upande wake uchunguzi wa " kuanzihwa kwa uasi" dhidi ya kundi la Wagner.

Mkuu wa kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, akitembea akiwa amejihami katika mitaa ya Rostov-on-Don.
Mkuu wa kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, akitembea akiwa amejihami katika mitaa ya Rostov-on-Don. AP
Matangazo ya kibiashara

"Tunaendelea, tutaenda hadi mwisho," amesema Yevgeny Prigozhin katika ujumbe wa sauti kwenye Telegram. "Tutaharibu chochote kitakachotuzuia," ameongeza.

Alitangaza kwamba majeshi yake, hadi sasa yaliyotumwa nchini Ukraine, "yamevuka (...) mpaka wa Urusi" na kuingia Rostov, kusini mwa nchi. Baadaye, amehakikisha kwamba askari wake waliangusha helikopta ya Urusi ambayo "ilifyatua risasi kwenye safu ya raia".

Hali ya wasiwasi yatanda katika mji wa mkuu wa Urusi, Moscow.
Hali ya wasiwasi yatanda katika mji wa mkuu wa Urusi, Moscow. © Ведомости

Hayo yanajiri wakati kuna uvumi unaosambaa Moscow kuhusu kutoroka kwa Vladimir Putin katika mji huo.

"Rais anafanya kazi Kremlin," anasema msemaji wake Dmitry Peskov, aliyenukuliwa na shirika la habari la serikali la Ria Novosti, ambalo lilimuuliza kuhusu uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii unaodai kwamba rais Putin aliondoka Moscow kwa sababu ya uasi wa kundi la Wagner.

Wakazi wa jimbo la Lipetsk watakiwa kusalia nyumbani

"Ili kuhakikisha utaratibu na usalama wa raia wa jimbo la Lipetsk, Halmashauri ya kikanda inatoa wito kwa wakazi wasiondoke manyumbani kwao isipokuwa kama kuna ulazima, na kukataa kusafiri kwa magari ya kibinafsi" , imebaini akaunti ya Telegram ya mamlaka ya jimbo hilo,  linalopatikana kilomita 420 kusini mwa Moscow. Wito huu unaambatana na matangazo kwenye Twitter ya video zinazoonyesha safu ya magari, baadhi yao yakiwa yamebeba mizinga, yakipita kwenye barabara ya shirikisho ya M4 kwenye eneo laa mji wa Horse-Kolodezsky, katika jimbo la Lipetsk.

Msafara wa Wagner unapita jiji la Voronezh kuelekea Moscow.

Ripota wa shirika la habari la Reuters anaripoti kuona msafara magari ya wapiganaji wa Wagner wakisafiri kutoka kusini mwa Urusi kuelekea Moscow, wakipita mji wa Voronezh. Angalau gari moja inabeba kifaru cha kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.