Pata taarifa kuu

Uasi wa Wagner: Baada Prigozhin kujirudi, mustakabali wa Shoigu na Guerassimov mashakani

Uasi wa Kundi la Wagner umesababisha taarifa chache kutoka kwa maafisa wa Urusi. Kati ya nchi wanachama kumi na wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni nchi tano tu zimetoa maoni juu ya hatua ya Yevgeny Prigozhin. Miongoni mwa viongozi mashuhuri, maafisa wawili ambao walikuwa wanalengwa na mkuu wa kundi la Wagner, ni Waziri wa Ulinzi, Sergei Choïgou, na Valéry Guerassimov, Mkuu wa jeshi.

Waziri wa Ulinzi (kushoto) Sergei Shoigu na Mkuu wa majeshi Jenerali Valery Gerasimov wakati wa mkutano na Vladimir Putin mnamo mwezi Desemba 2022.
Waziri wa Ulinzi (kushoto) Sergei Shoigu na Mkuu wa majeshi Jenerali Valery Gerasimov wakati wa mkutano na Vladimir Putin mnamo mwezi Desemba 2022. AP - Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Je, ipi hatima ya Sergei Choïgou, Waziri wa Ulinzi na Valéry Guerassimov, Mkuu wa jeshi? Wako wapi ? Hayo ni maswali ambayo waangalizi hujiuliza baada ya kundi la Wagner kusitisha hatua yake ya kuelekea Moscow. Kwa vyovyote vile, watu hao wawili wenye nguvu wa jeshi la Urusi hawakutoa taarifa yoyote kufuatia siku ya Jumamosi Juni 24.

Ikiwa hakuna chochote kilivuja juu ya makubaliano yaliyopatikana ili Yevgeny Prigozhin aweze kusitisha hatua yake, mkuu wa kundi la Wagner "labda alisisitiza juu ya mabadiliko katika jeshi katika suala la uongozi, anabaini mhariri mkuu wa Idhaa ya Kirusi ya RFI, Elsa Vidal. Prigozhin ni mtu ambaye, kwenye uongozi wa kundi la Wagner, alileta ushindi pekee ambao jeshi la Urusi liliweza kupata nchini Ukraine, na akahimiza kuondolewa kwa watu anaowaita wasaliti ambao ni waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa jeshi Valery Gerasimov. Kwa hivyo, itakuwa muhimu kufuata katika wiki zijazo mabadiliko yoyote kwa mkuu wa jeshi, lakini pia katika mbinu na malengo ya vita, "anaongeza.

Uzembe wa makao makuu ya jeshi

Kwa miezi kadhaa, Yevgeny Prigozhin amekuwa akiongeza ukosoaji wa maafisa hawa wawili, akiwashutumu kwa kutokuwa na uwezo katika kuendesha vita nchini Ukraine, na kudai kuuawa kwa maafisa hao wa ngazi ya juu katika jeshi. "Guerasimov na Shoigu lazima wawajibike kwa mauaji ya halaiki ya raia wa Urusi, na kuhamisha maeneo ya Urusi kwa adui," alisema mkuu wa Wagner kwenye kituo chake cha Telegram siku ya Ijumaa, akizindua uasi wake.

Sergei Shoigu alishinikiza kundi la Wagner kuwekwa chini ya udhibiti wake wa moja kwa moja, lakini aligonga ukuta. Mwanzoni mwa mwezi Juni, Waziri wa Ulinzi aliwataka wanamgambo wa Wagner kutia saini mkataba unaowaunganisha kwa jeshi la serikali kabla ya Julai 1. Sharti ambalo lilipingwana Yevgeny Prigozhin na hivyo kusababisha mvutano kati ya wawili hao.

Majina ya warithi wanaoweza kuchukuwa nafasi hizo yanazunguka

Kwa kuhitimisha makubaliano chini ya upatanishi wa Belarus Jumamosi jioni, Yevgeny Prigozhin alipata dhamana ya usalama pamoja na watu wake. Hawatafunguliwa mashtaka na Yevgeny Prigozhin ataondoka Urusi hivi karibuni kwenda Belarusi kama kwenda uhamishoni. Lakini mkuu wa Wagner pia anaweza kupata makubaliano juu ya mustakabali wa Waziri wa Ulinzi. Majina ya warithi wake tayari yanazunguka.

Miongoni mwao, jina la Alexei Dioumin, afisa mkuu wa FSB, afisa wa zamani wa idara ya usalama ya rais na gavana wa sasa wa mkoa wa Tula, linatajwa mara kwa mara. Uvumi hata unampa nafasi muhimu katika majadiliano ya jinsi ya kumaliza mzozo siku ya Jumamosi. Uvumi uliokanushwa na wale walio karibu naye kwa kuwa mazungumzo na Yevgeny Prigozhin hayako ndani ya uwezo wake, imehakikisha idara yake ya vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.