Pata taarifa kuu

Marekani: Tim Scott atarajia kuwa rais wa kwanza mweusi kutoka chama cha Republican

Seneta pekee mweusi wa chama cha Republican, Tim Scott, amezindua rasmi Ijumaa katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais nchini Marekani kwa mwaka 2024, ingawa kura za maoni zinampa 2% tu ya nia ya kupiga kura katika uchaguzi wa mchujo wa chama chake.

Seneta mweusi Tim Scott kutoka chama cha Republican, Marekani.
Seneta mweusi Tim Scott kutoka chama cha Republican, Marekani. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo aliyechaguliwa katika jimbo la South Carolina amewasilisha barua yake ya kugombea rasmi kwa Tume ya Uchaguzi ya Shirikisho na kuwatolea wito wafuasi wake kuandamana naye siku ya Jumatatu hadi Chuo Kikuu cha Charleston Southern kwa "tangazo maalum."

Mkristo huyu wa kiinjilisti mwenye umri wa miaka 57, ambaye anaweka imani yake kiini cha harakati zake za kisiasa, hajaficha matarajio yake ya urais katika miezi ya hivi karibuni.

Baada ya kuchaguliwa tena katika Baraza la Congress mwezi Novemba - akiwa na pointi 26 mbele ya mpinzani wake - hivyo alimtaja babu yake ambaye alimpigia kura Barack Obama. "Laiti angeishi muda wa kutosha kuona rais mwingine wa rangi na wakati huu alikuwa Republican!"

Akiwa na maadili ya kihafidhina juu ya uavyaji mimba au wajibu wa mtu binafsi, ananuia kujitofautisha na aliyekuwa Rais Donald Trump, kipenzi kikuu katika mchujo wa chama cha Republican, akiwa na ujumbe wa matumaini. "Familia za Marekani zinasubiri matumaini. Tunahitaji kuwa na imani. Imani kwa Mungu, ndani yetu wenyewe, Marekani," ameandika kwenye Twitter kabla ya kuzindua.

Katika chama ambacho kimesalia kutawaliwa na wazungu, nafasi yake ya kushinda inaonekana, katika hatua hii, ni finyu sana, huku 2% ya nia ya kupiga kura dhidi ya 56% ya Donald Trump, kulingana na kura za hivi punde.

Gavana wa Florida Ron DeSantis, ambaye anatarajiwa kujitangaza katikati ya wiki ijayo, amefikia 20%, na balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley kwa 4.3%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.