Pata taarifa kuu

Wapiga kura wa Georgia kumteua mwakilishi wao katika Bunge la Seneti la Shirikisho

Tarehe 6 Desemba Wakazi wa Georgia wanapiga kura kumchagua mwakilishi wao katika Bunge la Seneti la shirikisho nchini Maerekani. 

Hii ni duru ya pili katika jimbo la Georgia kumteua seneta atawawakilisha katika Bunge la Seneti huko Washington.
Hii ni duru ya pili katika jimbo la Georgia kumteua seneta atawawakilisha katika Bunge la Seneti huko Washington. © Ken Cedeno / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii ni duru ya pili katika jimbo la Georgia kumteua seneta atakayeketi Washington. Wapiga kura wana chaguo kati ya Raphaël Warnock wa chama cha Democrat na Herschel Walker wa chama cha Republican. 

Chama cha Democratic tayari kinaelekea kudhibiti Bunge la Seneti, lakini kinataka wingi zaidi wa viti.

Chama cha Democratic ambacho tayari kina viti 50 vinavyohitajika na kwa kura ya maamuzi ya Makamu wa Rais Kamala Harris endapo watashindana, Chama hiki cha Rais Joe Biden kinaelekea kupata kura nyingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.