Pata taarifa kuu
MAREKANI

Hatimaye Kevin McCarthy achaguliwa kuwa spika wa bunge nchini Marekani

Nchini Marekani, hatimaye Kevin McCarthy kutoka chama cha Republican, amechaguliwa kuwa spika wa bunge, baada ya jaribio la 15 kwa kipindi cha siku tatu zilizopita.

Spika mpya wa bunge la Marekani  Kevin McCarthy
Spika mpya wa bunge la Marekani Kevin McCarthy © REUTERS / EVELYN HOCKSTEIN
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ilikuja baada ya wabunge wa chama chake kulegeza msimamo na kumpigia kura na kupata ushindi wa kuea 216 dhidi ya mpînzani wake Hakeem Jeffries kutoka chama cha Democratic, aliyepata kura 212.

Baada ya ushindi huo, Spika McCarthy ameahidi kuwatumikia raia wa Marekani.

“Nitakuwa spika wa raia wa Marekani, sio chama changu,” alisema katika hotuba yake ya kwanza kama spika.

Rais Joe Biden amempongeza kwa ushindi huo, na kusema anatarajia ushirikiano na chama cha Republican katika siku zijazo.

" Niko tayari kushirikiana na chama cha Republican, pale itakapowezekana ili kutimiza maslahi ya Wamarekani," amesema Biden.

Hii ndio mara ya Kwanza kwa zoezi la kumchagua spika kuchukua muda mrefu katika historia ya bunge hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.