Pata taarifa kuu
MAREKANI

Wahamiaji 50 wapoteza maisha baada ya kupatikana ndani ya Lori nchini Marekani

Nchini Marekani miili ya wahamiaji 50 waliokuwa wameingia nchini Marekani  imepatikana ndani ya Lori katika mji wa Texas, huku ikiripotiwa kuwa watu hao walikuwa wametokea nchini Mexico, Guatemala na Honduras.

Laori lilokuwa limewabeba wahamiaji waliopatikana mjini Texas
Laori lilokuwa limewabeba wahamiaji waliopatikana mjini Texas via REUTERS - ABC AFFILIATE KSAT
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador amewalaumu walanguzi wa binadamu na ukosefu wa mipangilio mipakani kama sababu kuu ya janga hilo.

Aidha, amesema umasikini na kukosa tumaini, kumewasababishia maafa raia wake wapatao 12 waliokuwa wanakwenda kutafuta maisha mazuri nchini Marekani.

Wengine waliopoteza maisha ni pamoja na raia saba wa Guatemala na wawili kutolka nchini Honduras.

Waliopatiakana wakiwa hai ni pamoja na waririr wanne, waliokimbizwa hospitalini kupata matibabu.

Mwaka uliopita pekee, wahamiaji haramu 650 walipoteza maisha wakivuka mpaka kuelekea nchini Marekani kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa  Mataifa la uhamiaji IOM.

Tangu mwaka 2021 maafisa wa usalama nchini Marekani  wamewakamata wahamiaji haramu Milioni moja na Laki Saba hasa kutoka mataifa ya Amerika ya Kati, wakijaribu kuingia nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.