Pata taarifa kuu

Wavenezuela wafikia makubaliano ya kihistoria Mexico, Marekani yapongeza

"Mkataba wa pili wa sehemu ya ulinzi wa kijamii wa raia" uliweza kupatikana Jumamosi hii, Novemba 26 huko Mexico, kati ya mamlaka ya Venezuela na upinzani. Na katika mchakato huo, vikwazo vya Marekani vinavyoielemea sekta ya mafuta ya serikali ya Caracas vimeanza kuondolewa. Washington imeidhinisha kampuni ya mafuta ya Chevron kuanza kwa sehemu shughuli zake za uchimbaji mafuta katika nchi ya Nicolas Maduro.

Kutoka kushoto kwenda kulia: Mjumbe wa upinzani wa Venezuela Gerardo Blyde Pérez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Marcelo Ebrard, mwanadiplomasia wa Norway Dag Nylander na Spika wa Bunge la Venezuela, Jorge Rodriguez, Jumamosi hii, Novemba 26 nchini Mexico.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Mjumbe wa upinzani wa Venezuela Gerardo Blyde Pérez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Marcelo Ebrard, mwanadiplomasia wa Norway Dag Nylander na Spika wa Bunge la Venezuela, Jorge Rodriguez, Jumamosi hii, Novemba 26 nchini Mexico. AP - Fernando Llano
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa,Wizara ya Fedha ya Marekani imetangaza kwamba kampuni kubwa ya Chevron imeidhinishwa kuzindua kwa sehemu shughuli zake za uchimbaji mafuta nchini Venezuela, kwa ushirikiano na kampuni ya Petróleos ya nchini Venezuela (PdVSA), kwa masharti kwamba "PdVSA haipati mapato yoyote kutoka uuzaji wa mafuta wa Chevron.

Uamuzi huu ulitolewa baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya sehemu kati ya serikali ya chama cha United Socialist Party of Venezuela (PSUV) na upinzani nchini Mexico, na wakati Marekani inatafuta hidrokaboni mbadala kutokana na hasara ya mafuta ghafi ya Kirusi, kutokana na vikwazo vilivyopitishwa tangu vita vya Ukraine.

Mazungumzo kati ya Venezuela yalianza tena Ijumaa katika Jiji la Mexico, wakati Caracas ni mwenyeji, tangu Jumatatu, wa mazungumzo yaliyonzishwa tena kati ya serikali ya Bogota na waasi wa Jeshi la Ukombozi wa Kitaifa (ELN). Mchakato wa sasa ulianza mwezi wa Agosti 2021 nchini Mexico, lakini Bw. Maduro aliusimamisha miezi miwili baadaye.

Wawakilishi wa rais aliyekashifiwa Maduro walitangaza makubaliano hayo mchana wa Jumamosi. Mnamo Mei, serikali ya Marekani iliiruhusu Chevron "kujadili masharti ya shughuli zinazowezekana za baadaye nchini Venezuela", kuondolewa kwa moja ya vikwazo vya mafuta vya Venezuela vilivyowekwa na Washington mnamo 2019.

Katika majadiliano haya, rais wa Venezuela alitarajia kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani kwa nchi yake, na hasa vikwazo vya mauzo ya mafuta nje ya nchi. Upinzani ulidai suluhu kwa mzozo wa kibinadamu, kuheshimiwa kwa haki za binadamu na dhamana ya uchaguzi huru na unaoonekana.

Afisa mkuu wa Marekani alielezea makubaliano hayo, kulingana na shirika la habari la AFP, kama hatua muhimu katika mwelekeo sahihi. Mazungumzo haya yanajumuisha "tumaini kwa Amerika ya Kusini" na "ushindi wa siasa", alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Marcelo Ebrard.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.