Pata taarifa kuu

Mexico: Mwanasheria mkuu wa zamani akamatwa kwa kutoweka kwa wanafunzi 43 Ayotzinapa

Baada ya ripoti ya tume ya serikali kuitaja kesi hiyo "uhalifu wa serikali", vyombo vya sheria nchini Mexico siku ya Ijumaa Agosti 19, 2022, vilimkamata mwanasheria mkuu wa zamani wa nchi hiyo na kuamuru kukamatwa kwa polisi 64 na wanajeshi kwa kutoweka mnamo 2014 kwa wanafunzi 43 kutoka shule ya ya upili ya Ayotzinapa, kusini mwa nchi. Huyu ndiye mtu muhimu zaidi aliyekamatwa katika kesi hiyo, ambayo ilianza tena kutoka mwanzo baada ya Andrés Manuel Lopez Obrador kuchukuwa mamlaka ya urais.

Maafisa wa polisi wa Mexico wakilinda lango la ofisi ya mwanasheria mkuu wa Mexico, ambako Jesus Murillo alikuwa akishikiliwa na kusikizwa na mahakama kuhusiana na uchunguzi wa kutoweka kwa wanafunzi 43 mwaka 2014, huko Maxico, Agosti 19, 2022.
Maafisa wa polisi wa Mexico wakilinda lango la ofisi ya mwanasheria mkuu wa Mexico, ambako Jesus Murillo alikuwa akishikiliwa na kusikizwa na mahakama kuhusiana na uchunguzi wa kutoweka kwa wanafunzi 43 mwaka 2014, huko Maxico, Agosti 19, 2022. © Luis Cortes / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa jioni, mwanasheria mkuu wa zamani Jesus Murillo Karam alikamatwa nyumbani kwake huko Mexico kwa "kutoweka, kuteswa na uhalifu dhidi ya utawala wa vyombo vya habari", na hakuweka upinzani wowote, imesema ofisi ya mwendesha mashtaka katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Baadaye ilitangaza kwamba vibali vya kukamatwa vimetolewa dhidi ya maafisa 20 wa jeshi, maafisa wa polisi 44 na watumishi wa umma watano kwa madai ya kuhusika katika tukio hili, ambalo lilisababisha mshtuko mkubwa nchini Mexico na nje ya nchi.

Maafisa hawa wa polisi na askari 64 wanatafutwa kwa "uhalifu wa kupangwa, mateso, mauaji na makosa dhidi ya utendaji wa haki", ulibainisha upande wa mashtaka.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jesus Murillo Karam alikuwa amehudumu chini ya Rais Enrique Peña Nieto (2012-2018) na aliongoza uchunguzi wa kwanza wenye utata kuhusu kutoweka kwa watu hawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.