Pata taarifa kuu

Joe Biden azitaka nchi za Amerika kuimarisha demokrasia kwa ajili ya mafanikio

Rais wa Marekani amebaini kwamba demokrasia ni 'muhimu kwa mustakabali wa bara la Amerika,' katika hafla ya ufunguzi huko Los Angeles iliyoangaziwa na nyimbo na jumbe kutoka kwa watoto wanaopongeza nchi za Amerika kwa rasilimali zao.

Rais wa Marekani Joe Biden alifungua Mkutano wa 19 wa nchi za Amerika Jumatano jioni Juni 8 huko Los Angeles.
Rais wa Marekani Joe Biden alifungua Mkutano wa 19 wa nchi za Amerika Jumatano jioni Juni 8 huko Los Angeles. AFP - JIM WATSON
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano Joe Biden alisisitiza juu ya hitaji la kutetea demokrasia na kushirikiana kwa ustawi zaidi wa kiuchumi, katika ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Amerika uliogubikwa na mizozo ya kidiplomasia. “Bara letu ni kubwa na lina watu kutoka makabila mbalimbali. Hatukubaliani kila wakati kwa kila kitu. Lakini kwa sababu sisi ni wanademokrasia, tunashughulikia tofauti zetu kwa kuheshimiana na mazungumzo,” alisema.

"Kosa la kimkakati"

Mkutano huo wa kilele wa kikanda ulishuhudia kukosekana kwa baadhi ya wakuu wa nchi, hasa kutoka Mexico, Guatemala, Bolivia na Honduras. Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador hasa ameikosoa Ikulu ya White House kwa kuzitenga Cuba, Nicaragua na Venezuela. Aliamua kutohudhuria mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico, Marcelo Ebrard, ambaye alishiriki mkutano, aliwaambia wenzake kwamba kutengwa kwa nchi hizi tatu ni "kosa la kimkakati". Pia alisema kuwa Mexico itachunguza jinsi ya kurekebisha taasisi za kikanda.

Joe Biden pia alipendekeza Jumatano kuzinduliwa kwa "Ushirikiano wa Amerika kwa Ustawi wa Kiuchumi" ili kuhimiza ukuaji jumuishi zaidi katika Amerika ya Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.