Pata taarifa kuu

Haiti: Muhula wa rais aliyeaga dunia wamalizika, nchi yaendelea kuzama kwenye mzozo

Tarehe 7 Februari ilipaswa kuwa siku ya makabidhiano ya mamlaka nchini Haiti, lakini miezi saba baada ya kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse, nchi hiyo inazidi kuzama katika mgogoro kwa sababu hakuna chombo au utawala unaoweza kusimamia kihalali mamlaka na migawanyiko kati ya kambi za kisiasa inaendeudiwa.

Mtu huyu akiwa ameshikilia picha ya rais wa Haiti aliyeuawa Jovenel Moise, wakati wa mazishi yake nyumbani kwa familia yake huko Cap-Haitien, Julai 23, 2021.
Mtu huyu akiwa ameshikilia picha ya rais wa Haiti aliyeuawa Jovenel Moise, wakati wa mazishi yake nyumbani kwa familia yake huko Cap-Haitien, Julai 23, 2021. REUTERS - RICARDO ARDUENGO
Matangazo ya kibiashara

Februari 7 ingelikuwa tarehe ya kukabidhiana madaraka kati ya rais Jovenel Moïse na mrithi wake, rais huyu aliuawa kabla ya kumaliza muhula wake. N a angemaliza muhula wake ilikuwa ishara muhimu ka taifa hilo.

Siku hii, mwaka wa 1986, ndipo udikteta wa Duvaliers ulifikia mwisho. Lakini kwa vile, katika kipindi cha chini ya miaka 40, katika tarehe hii ya msingi ya kumbukumbu ya demokrasia, Haiti tayari imejikuta mara nne bila rais aliyechaguliwa madarakani.

Tangu kuuawa kwa Jovenel Moïse mnamo Julai 7, hakuna aliye na uhalali wa kusimamia mamlaka. Baada ya uchaguzi uliofanyika tangu 2016, Bunge halifanyi kazi vizuri.

Wanasiasa waliogawanyika

Ariel Henry alikuwa ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu siku mbili kabla ya shambulio hili lakini hapata wakati wa kutawadhwa rasmi katika majukumu yake. Kwa sasa ni kiongozi wa serikali lakini wapinzani wake wanakashifu uhusiano ambao alikuwa nao, usiku wa mauaji ya rais, na mtu anayedaiwa kuwa mmoja washiriki wa mauaji hayo.

Hata hivyo, mikataba kadhaa ya utatuzi wa migogoro ipo, lakini wanasiasa wanaendelea kugawanyika. Haiti sasa inaingia katika utawala mpya wa mpito ambao usioeleweka na ambao bado haujawasilisha ratiba yoyote, mbele ya magenge ambayo yanazidisha mauaji na utekaji nyara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.