Pata taarifa kuu

Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa binadamu nchini Marekani

Kwa mara ya kwanza duniani,  nchini Marekani, Madaktari wa upasuaji wamefanikiwa kupandikiza moyo kutoka kwa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba hadi kwa binadamu mgonjwa, Chuo Kikuu cha tiba ya Maryland kimesema.

Katika picha hii iliyotolewa na Chuo cha kikuu cha Tiba cha Maryland, timu ya upasuaji inaonyesha moyo wa nguruwe tayari kupandikizwa kwenye mgonjwa David Bennett, Januari 7, 2022.
Katika picha hii iliyotolewa na Chuo cha kikuu cha Tiba cha Maryland, timu ya upasuaji inaonyesha moyo wa nguruwe tayari kupandikizwa kwenye mgonjwa David Bennett, Januari 7, 2022. via REUTERS - UMSOM
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ilitekelezwa siku ya Ijumaa. Ilionyesha, kwa mara ya kwanza, kwamba moyo wa mnyama unaweza kuendelea kufanya kazi kwa binadamu bila usumbufu wowote, Chuo Kikuu cha Maryland kimeongeza.

David Bennett, 57, ambaye alipokea moyo wa nguruwe, alitangazwa kuwa hastahili kupokea upandikizaji wa moyo wa binadamu. Sasa anafuatiliwa kwa karibu na madaktari ili kuhakikisha kiungo kipya kinafanya kazi vizuri.

"Yaani yalikuwa mambo mawili kwa binadamu huyo,  ima kifo au upandikizaji wa moyo wa nguruwe. Nataka kuishi. Ninajua ilinigusa sana, lakini ilikuwa chaguo langu la mwisho, "mkazi wa Maryland alisema siku moja kabla ya upasuaji wake, kulingana na chuo kikuu cha matibabu. "Siwezi kungoja niweze kuamka kitandani mara tu ninapokuwa mzima," David Bennett, ambaye amelala kitandani kwa miezi michache iliyopita na kutumia mashine inayomfanya aendelee kuishi.

Nguruwe aliyebadilishwa vinasaba

Mamlaka ya Madawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha operesheni hiyo jioni ya siku ya kuamkia Mwaka Mpya. "Haya ni mafanikio makubwa ya upasuaji na ambayo yanatuwezesha kupata suluhisho dhidi ya uhaba wa viungo, " amebaini Bartley Griffith, aliyefanyiwa upandikizaji wa moyo wa nguruwe.

Nguruwe ambao moyo hutoka umebadilishwa vinasaba ili kutozalisha tena aina ya sukari ambayo kwa kawaida iko kwenye seli zote za nguruwe na ambayo husababisha kiungo kukataa kufanya kazi mara moja. Marekebisho haya ya jeni yalifanywa na kampuni ya Revivicor, ambayo pia ilitoa figo ya nguruwe ambalo madaktari wa upasuaji walifanikiwa kuunganisha kwa mishipa ya damu ya mgonjwa aliyekuwa mahututi huko New York mwezi Oktoba.

Takriban Wamarekani 110,000 kwa sasa wako kwenye orodha ya wanaosubiri kupandikizwa viungo na zaidi ya watu 6,000 wanaohitaji upandikizaji hufa kila mwaka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.