Pata taarifa kuu

Marekani yamteua David Satterfield kuwa mjumbe mpya katika Pembe ya Afrika

Mtaalamu huyu wa Mashariki ya Kati, balozi wa zamani wa Ankara, atachukua wadhifa wake "katika siku chache zijazo," waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema katika taarifa yake siku ya Alhamisi (tarehe 7 Januari). Anachukua nafasi ya Jeffrey Feltman ambaye amejiuzulu kwenye wadhifa wake kutokana na hali ya mzozo wa Ethiopia na mgogoro wa Sudan.

Mwanadiplomasia wa Marekani David Satterfield, Julai 12, 2019, mjini Ankara, alipokuwa balozi nchini Uturuki.
Mwanadiplomasia wa Marekani David Satterfield, Julai 12, 2019, mjini Ankara, alipokuwa balozi nchini Uturuki. AP - Burhan Ozbilici
Matangazo ya kibiashara

Miezi tisa baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Pembe ya Afrika, Jeffrey Feltman amejiuzulu baada ya kukumbwa na matatizo makubwa.

Kwanza kabisa kwenye faili ya Ethiopia. Zaidi ya mwaka mmoja baada ya mzozo kuanza kati ya serikali ya Addis Ababa na waasi huko Tigray, juhudi za kidiplomasia za Marekani hazikufaulu: mjumbe wa zamani wa Marekani alishindwa kukabiliana na mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na waasi kutoka Tigray. Na hali ya kibinadamu katika eneo la Tigray inachukuliwa kuwa ya kutisha.

Kushindwa pia nchini Sudan ambako Jeffrey Feltman alikumbana na hali nzito mwezi Oktoba mwaka jana, wakati utawala wa kijeshi ulipomfukuza waziri mkuu wa kiraia na kuchukua madaraka, saa chache baada ya kuondoka kwa mjumbe wa Marekani kutoka mji mkuu wa Sudan. Ingawa aliamini kuwa amepata uhakikisho wa kuridhisha kutoka kwa jeshi.

Anthony Blinken anasema mjumbe anayeondoka kila mara alikuwa na nia ya kuondoka baada ya chini ya mwaka mmoja. Na ameongeza kuwa atasalia kuwa mshauri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.