Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani yaziondoa Ethiopia, Mali na Guinea katika mkataba wa kibiashara wa Agoa

Utawala wa Joe Biden ulitangaza Jumamosi hii, Januari 2, kuwa umeziondoa Ethiopia, Mali na Guinea kutoka Agoa, mkataba wa kibiashara unaoiunganisha Marekani na Afrika. Washington imeamua kuwa hatua zinazochukuliwa na serikali hizi tatu zinakiuka kanuni.

Guinea, Mali na Ethiopia zimeondolewa katika Agoa, mkataba wa biashara huria kati ya Marekani na Afrika.
Guinea, Mali na Ethiopia zimeondolewa katika Agoa, mkataba wa biashara huria kati ya Marekani na Afrika. AFP PHOTO / Karen BLEIER
Matangazo ya kibiashara

"Marekani leo imezionda Ethiopia, Mali na Guinea katika mpango wa upendeleo wa kibiashara wa Agoa kwa sababu ya hatua zilizochukuliwa na kila moja ya serikali zao kinyume na sheria" za makubaliano haya, umibaini Uwakilishi wa Biashara wa Marekani (USTR) katika taarifa.

Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika ni makubaliano ya kibiashara yaliyowekwa mwaka 2000 chini ya utawala wa Clinton ili kuwezesha na kudhibiti biashara kati ya Marekani na Afrika.

Mabadiliko kinyume na katiba na haki za binadamu

"Utawala wa Biden na Harris una wasiwasi mkubwa kuhusu mabadiliko yasiyo ya kikatiba ya serikali za Guinea na Mali," inaelezwa katika taarifa.

Aidha, utawala una wasiwasi kuhusu "ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu zinazotambulika kimataifa, unaofanywa na serikali ya Ethiopia na vyama vingine katika mzozo unaoenea kaskazini mwa Ethiopia," ilisema taarifa hiyo.

"Kila nchi ina alama za wazi za njia ya kuunganishwa tena na utawala wa Marekani utafanya kazi na serikali zao kufikia lengo hili," inasema USTR.

Chini ya Mkataba wa Agoa, maelfu ya bidhaa za Kiafrika zinaweza kunufaika kutokana na kupunguzwa kwa kodi kutoka nje. Lakini makubaliano haya yanawezekana tu kwa kuzingatia masharti yanayotimizwa kuhusu haki za binadamu, utawala bora na ulinzi wa wafanyakazi na vile vile kutotumia marufuku yoyote ya forodha kwa bidhaa za Marekani kwenye eneo lao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.