Pata taarifa kuu
MAREKANI-JAMII

Joe Biden akaribisha takwimu za ajira

Ingawa idadi ya jumla ya nafasi za ajira, chini ya 200,000 tu kwa mwezi wa Desemba, inakatisha tamaa wachambuzi, Rais Joe Biden ameridhika kikamilifu kwa mwaka wake wa kwanza wa uongozi kwa uchumi wa Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House, Januari 7, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House, Januari 7, 2022. REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

Licha ya takwimu zilizochanganyika za mwezi wa Desemba, na ubunifu wa kazi unaokatisha tamaa, Rais wa Marekani alionyesha kuridhika kwake jana Ijumaa Januari 7 kuona ukosefu wa ajira ukirudi katika kiwango chake cha kabla ya janga la Covid-19 (3.5%).

"Leo hii kiwango cha ukosefu wa ajira katika ngazi ya kitaifa kimeshuka chini ya 4% hadi 3.9%. Huku ni kupungua kwa kasi zaidi kwa ukosefu wa ajira katika mwaka mmoja katika historia ya Marekani, Joe Biden alisema wakati wa hotuba yake kutoka Ikulu ya White House. Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 ambapo kiwango cha ukosefu wa ajira kimeshuka chini ya 4% katika mwaka wa kwanza wa muhula wa rais. 3.9% ya kiwango cha ukosefu wa ajira, miaka kadhaa kabla ya kile ambacho wataalam walitabiri. "

Lakini Marekani ambayo ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani ilitoa ajira 199,000 pekee mwezi Desemba 2021, mbali na 440,000 zinazotarajiwa na wachambuzi wakati soko la ajira likikabiliana na wimbi la maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.