Pata taarifa kuu

Biden amshutumu Trump kwa "kujaribu kuzuia zoezi la kukabidhiana madaraka kwa amani"

Mwaka mmoja baada ya shambulio la makao makuu ya Bunge la Marekani, Capitol Hill, Rais wa Marekani Joe Biden ametoa hotuba Alhamisi, Januari 6, ambapo anamshtumu mtangulizi wake Donald Trump.

Rais wa Marekani Joe Biden kkatika jengo la makao makuu ya Bunge, Capitol Hill, Januari 6, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden kkatika jengo la makao makuu ya Bunge, Capitol Hill, Januari 6, 2022. AP - Drew Angerer
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba kutoka Capitol Hill, mahali ambapo wafuasi wa Donald Trump walijaribu kuzuia uchaguzi wake kuthibitishwa mwaka mmoja uliopita, Joe Biden amemshamlbulia kwa maneno mtangulizi wake bila hata kumtaja. Rais huyo kutoka chama cha Democratic, mwenye umri wa miaka 79 ametumia vifungu vya maneno, kama vile "rais wa zamani" au "rais wa zamani aliyeshindwa".

Joe Biden amemshutumu bilionea huyo wa chama cha Republican kwa "kujaribu kuzuia zoezi la kukabidhiana madaraka kwa amani" wakati wa "uasi ulioendeshwa na watu wenye silaha" Januari 6, 2021. Donald Trump "aliunda na kueneza uwongo kuhusu uchaguzi wa mwaka 2020, alifanya hivyo , kwa sababu alipendelea mamlaka kuliko kanuni ", na kwa sababu" ubinafsi wake ni muhimu zaidi kwake kuliko demokrasia yetu ", amesema Rais Joe Biden, ambaye alikuwa hajawahi kufanya mashambulizi kama haya dhidi ya mtanguliziwake.

Jibu la Donald Trump halikuchukua muda mrefu: bilionea huyo amebaini kwamba hotuba ya mrithi wake, ambaye kiwango chake cha kuungwa mkono na kuaminiwa na wananchi kimeshuka, ilikuwa ni " michezo wa kuigiza wa kisiasa"  iliyokusudia kugeuza tahadhari ya "kushindwa" kwake.

"Je, tutakuwa taifa linalokubali vurugu za kisiasa kama kawaida? (...) Je, tutakuwa taifa ambalo haliishi katika nuru ya ukweli, bali katika kivuli cha uongo? Joe Biden ameuliza. "Hatuwezi kumudu kuwa taifa la aina hiyo," amesema, akibaini kwamba Marekani ilijikubalisha, ndani na nje ya mipaka yake, katika "mapambano" kati ya demokrasia na utawala wa kiimla. "Sikutaka kufuta vita hivi," amekiri Joe Biden, wakati kulingana na kura ya maoni ya hivi majuzi, ni 55% tu ya Wamarekani waliamini kuwa kuchaguliwa kwake ni halali. Lakini "Sitamruhusu mtu yeyote kuvunja demokrasia ya Marekani", ameonya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.