Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Shambulio Capitol Hill: Trump apata afueni kuhusiana na kesi dhidi yake

Hati ambazo zinaweza kumhusisha Donald Trump katika tukio la shambulizi dhidi ya makao makuu ya Bunge Capitol Hill Januari 6 mwaka huu zinatarajiwa kutumwa kwa Baraza la Wawakilishi leo Ijumaa.

Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani huko Washington, Agosti 8, 2021.
Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani huko Washington, Agosti 8, 2021. MANDEL NGAN AFP
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani aliomba Mahakama ya Marekani isitishe kwa muda uchapishaji wa nyaraka za White House ambazo zinaweza kumhusisha na shambulio la Januari 6 dhidi ya Capitol. Hati hizi zimeombwa na kamati maalum ya Baraza la Wawakilishi inayochunguza shambulio hilo, na uchapishaji wao uliamriwa Jumanne na jaji wa shirikisho kwa jina la "maslahi ya umma" kuelewa "matukio ambayo yalisababisha kufanyika kwa shambulio hilo Januari 6 ". Lakini mahakama ya Marekani ilikubali Alhamisi, Novemba 11 kwa ombi la Donald Trump.

Baada ya mawakili wa bilionea huyo kuhojiwa, Mahakama ya Rufaa ilisema Alhamisi kuwa ilitoa "amri ya kiutawala" na kupanga kuwa kesi hiyo itasikilizwa Novemba 30. Mahakama hiyo, inayojumuisha majaji watatu, ilisema uamuzi huo "usifasiriwe kwa vyovyote kuwa uamuzi juu ya uhalali" wa kesi hiyo.

Joe Biden alikuwa ametoa idhini yake

Januari 6, maelfu ya wafuasi wa Donald Trump walikuwa wamekusanyika Washington wakati Bunge la Congress lilithibitisha ushindi wa mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Joe Biden, katika uchaguzi wa urais wa Novemba 2020. Donald Trump alihutubia umati, akisisitiza, bila msingi, kwamba uchaguzi "uliibiwa" kutoka kwao. Mamia kadhaa ya waandamanaji kisha walivamia ofisi ya chama cha Democratic, na kusababisha machafuko na vurugu hata katika makao makuu ya Bunge.

Joe Biden tayari ametoa idhini yake kwa uchapishaji wa baadhi ya kurasa 770 za hati ambazo zimehifadhiwa katika Maktaba ya Kitaifa, ambayo sehemu yake ilipaswa kutumwa kwa Congress leo Ijumaa. Zinajumuisha faili za washauri wa karibu wa Donald Trump na jarida la kila siku la White House - akaunti ya shughuli zake, safari, maelezo mafupi na simu.

Nyaraka zingine ambazo rais huyo wa zamani hataki Bunge zione ni pamoja na barua aliyowasilisha kwa katibu wake wa zamani wa masuala ya habari Kayleigh McEnany, barua iliyoandikwa kwa mkono kuhusu matukio ya Januari 6, na mswada wa hotuba yake katika mkutano wa Save America, uliotangulia shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.