Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Bunge la Marekani afungua uchunguzi juu ya shambulio la Capitol Hill

Zaidi ya miezi sita baada ya shambulio dhidi ya makao makuu ya Bunge, Capitol Hill, huko Washington, kamati ya bunge, inaanzisha Jumanne wiki hii uchunguzi kuhusu mgogoro huu mkubwas kwa demokrasia ya Marekani, katika hali mbaya ambayo inaweza kuhatarisha shughuli zake

Waandamanaji wanaomuunga mkono Trump wakikusanyika mbele ya makao makuu ya Bunge, Capitol, Januari 6, 2021.
Waandamanaji wanaomuunga mkono Trump wakikusanyika mbele ya makao makuu ya Bunge, Capitol, Januari 6, 2021. AP - Manuel Balce Ceneta
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa polisi watakuwa wa kwanza kuhojiwa na kundi la wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi lililopewa jukumu la kutafuta"ukweli" juu ya shambulio la Januari 6.

Baada ya mvutano wa kisiasa, tume hii ina wapinzani kutoka kwa rais wa zamani Donald Trump, hali ambayo "haionyeshi vizuri kama kweli uchunguzi utaendeshwa vizuri" na itaharibu "uaminifu" wake, kulingana na kiongozi wa chama cha Republican katika Bunge hilo Kevin McCarthy.

Kevin McCarthy ndiye ambaye anasusia shughuli za Bunge, amesema Spika wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Democratic, Nancy Pelosi. "Labda wa wabunge wa chama cha Republican hawawezi kukabili ukweli, lakini tuna jukumu la kuutafuta, na kuupata," amesema.

Wademocrats na Republicans walikuwa bado wana hofu baada ya kuingiliwa kwa mamia ya wafuasi wa Donald Trump katika makao makuu ya Bunge, wakati wabunge walipothibitisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa urais.

Viongozi wa vyama hivyo viwili walilaani vikali shambulio hilo, ambapo Kevin McCarthy hadi kufikia hatua ya "kumuhusisha" Donald Trump kwa tukio hilo ambaye alidai mbele ya umati wa watu kuwa uchaguzi huo uligubikwa na "udanganyifu mkubwa" kabla ya tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.