Pata taarifa kuu
MAREKANI

Trump apigwa marufuku kutuma ujumbe wowote Facebook

Bodi ya usimamizi ya Facebook imeamua leo Jumatano kushikilia uamuzi wa mtandao  huo kumpiga marufuku rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook na akaunti yake ya Instagram.

Donald Trump alipigwa marufuku kurusha jumbe zake kwenye Facebook na Instagram baada ya kurusha video wakati wa machafuko ya Januari 6 yaliyotekelezwa na wafuasi wake kwenye makao makuu ya Bunge Capitol Hill, huku akisema: "Ninawapenda, ni watu bora".
Donald Trump alipigwa marufuku kurusha jumbe zake kwenye Facebook na Instagram baada ya kurusha video wakati wa machafuko ya Januari 6 yaliyotekelezwa na wafuasi wake kwenye makao makuu ya Bunge Capitol Hill, huku akisema: "Ninawapenda, ni watu bora". Olivier DOULIERY AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Bodi ya usimamizi inaamini, hata hivyo, kwamba "haikuwa sawa kwa Facebook kuweka" vikwazo vya muda usiojulikana na inaiomba "ifikirie tena uamuzi wa kiholela uliochukuliwa Januari 7" katika miezi sita ijayo, imeongezea katika taarifa.

Bodi ya usimamizi ya Facebook, ambayo maamuzi yake yana nguvu, imeamua kwamba Donald Trump "alikuwa ameweka mazingira ambapo kungelizuka hatari kubwa ya vurugu" pamoja na maoni yake Januari 6, siku ya shambulio dhidi ya makao makuu ya Bunge, Capitol Hill.

"Wakati wa kuchapishwa kwa jumbe za Bwana Trump, kulikuwa na hatari ya wazi na ya haraka ya kutokea vurugu na maneno yake ya kuunga mkono wale waliohusika katika ghasia hizo yalihalalisha vitendo vyao vya vurugu," bodi ya usimamizi ya Facebook imebaini.

Trump kushawishi wafuasi wake

Kama rais, Bwana Trump alikuwa na ushawishi mkubwa, pia imesema. "urushwaji wa jumbe zake ulikuwa muhimu, kwa watu milioni 35 wanaomfuata kwenye Facebook na milioni 24 kwenye Instagram," imeongeza.

Bodi ya usimamizi ya Facebook pia imetoa mapendekezo ya sera kutekelezwa na Facebook "kukuza sera zilizo wazi, zinazohitajika na sawia ambazo zinakuza usalama wa umma na kuheshimu uhuru wa kujieleza".

Mkurugenzi wa zamani wa Trump, Mark Meadows amelaani hatua hiyo, akisema ina athari mbaya kwa uhuru wa kujieleza na kutaka sheria kali zifuate au kuvunjwa kwa mtandao huo wa Facebook.

"Ni siku ya huzuni kwa Marekani, ni siku ya kusikitisha kwa Facebook," amesema kwenye kituo cha Fox News.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.