Pata taarifa kuu
MAREKANI

Democrats wataka Republican kuwaunga mkono katika kumkuta na hatia Trump

Baraza la wawakilisha hatimaye limekamilisha hoja zake za kumshtaki rais wa zamani wa Marekani DonaldTrump. Kwa muda wa siku tatu mfululizo, walionyesha jopo la majaji kuwa rais huyo wa zamani ni tishio kwa demokrasia nchini Marekani.

Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi.
Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Walijaribu kuonyesha kwamba walijua kabisa kwamba uwongo wake na matamshi yake makali yatasababisha wafuasi wafuasi wake kufanya vurugu Januari 6.

"Trump alijua hasa kile alichokuwa akifanya kwa kuchochea umati wa wafuasi wake Januari 6," amesema Jamie Raskin.

Wademocrats wameonya kuwa Donald Trump "anaweza kufanya hivyo tena" ikiwa hatatiwa hatiani.

Wademocrats pia waliwasilisha ushahidi kutoka kwa polisi, wafanyakazi, maafisa wa ujasusi na vyombo vya habari vya kigeni. Sasa ni zamu ya mawakili wa utetezi kuanza kutoa hoja zao leo Ijumaa.

Theluthi mbili zinahitajika kumtia hatiani Bw. Trump katika Bunge la Seneti lenye viti 100, lakini kuna uwezekano kusamehewa kama idadi kubwa ya maseneta wa Republican wameendelea kuwa waaminifu kwake hadi sasa.

Ikiwa Bw Trump atapatikana na hatia, hata hivyo, Baraza la Seneti pia linaweza kupiga kura kumzuia kushika wadhifa wa kuchaguliwa tena.

Baada ya kuagizwa na Trump kuandamana kuelekea bunge, ambako wabunge wakati huo walikuwa wanaidhinisha ushindi wa Biden, kundi la wafuasi wa Trump walivunja vizuwizi vya polisi, na kuanza kufanya uhairibifu mkubwa, watu watano walipoteza maisha wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.