Pata taarifa kuu
MAREKANI

Trump kutangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa 2024

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumanne ziki hii kuwa ataamua iwapo atawania tena au la kiti cha urais baada ya uchaguzi katika Bunge la congress uliopangwa kufanyika mnamo Novemba 2022.

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump.
Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump. AP - Carolyn Kaster
Matangazo ya kibiashara

Hapo awali Donald Trump alifahamisha kwamba anataka kuwasaidia wenzake wa Republican kupata udhibiti wa mabunge yote mawili  katika uchaguzi wa mwaka ujao, ambao utatumika kama kura ya maoni ya mapema juu ya muhula wa mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden, ambaye yuko mamlakani tangu Januari 20.

"Tuna nafasi nzuri sana ya kuchukua Baraza (la Wawakilishi)," amesema katika mahojiano na kituo cha Fox News. "Kuna nafasi nzuri ya kuchukua Bunge la Seneti na, kusema ukweli, tutafanya uamuzi wetu baada ya hapo," ameongeza Donald Trump.

Hotuba ya Donald Trump katika mkutano mkuu wa wawaconservatives.

Amesema wafuasi wake bado wanaonekana kuwa tayari kumuunga mkono ikiwa atawania katika uchaguzi wa urais mnamo Novemba 2024. "Kulingana na kura zote wanataka nigombee tena, lakini tutaangalia," amesema Donald Trump.

Hata hivyo, Bw. Trump ametoa wito kwa watu kukubali kuchanjwa dhidi ya Corona, kwani uchunguzi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapiga kura wa chama cha Republican na wafuasi wa Trump hawataki chanjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.