Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA-HAKI

Marekani: Watu 300 wakabiliwa na mashitaka baada ya kufanya uvamizi dhidi ya Capitol

Wizara ya Sheria ya Marekani imewashtaki zaidi ya watu 300 walioshiriki katika shambulio dhidi ya jengo la Bunge la Capitol Hill, shambulio lililotekelezwa na wafuasi wa rais wa zamani Donald Trump mnamo Januari 6, ambapo watu 280 walikamatwa, afisa mmoja wenye wizara hiyo amesema.

Hatua ya mamia ya wafuasi wa rais wa Marekani Donald Trump kuyavamia majengo ya Bunge la Marekani, maarufu kama Capitol Hill mjini Washington, imesababisha maoni mengi kutolewa kote duniani.
Hatua ya mamia ya wafuasi wa rais wa Marekani Donald Trump kuyavamia majengo ya Bunge la Marekani, maarufu kama Capitol Hill mjini Washington, imesababisha maoni mengi kutolewa kote duniani. Joe Raedle POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Uchunguzi unaendelea kwa kasi isiyokuwa ya kawaida, na hivyo ndivyo ilivyo," Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali John Carlin amesema.

Wale waliohusika na shambulio hili lazima wawajibishwe

.

Siku ya IJumaa shirika la ujasusi la Marekani la FBI lilitangaza kuwa limeimarisha hatua za kiusalama kwenye jumba la Capitol kabla ya hotuba rais Joe Biden  anajiandaa kutoa kuhusu muungano, kwa kuhofia shambulio.

Takriban watu wanne wamefariki nchini Marekani baada ya waandamanaji wanaomuunga mkono rais Trump kuvamia bunge na kuzuia kuidhinishwa kwa Joe Biden kuwa mshindi wa uchaguzi uliopita Marekani.

Wafuasi wa Trump waliokuwa na hasira waliandamana huku wakiimba, "Tunamtaka Trump".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.